28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

‘WATANZANIA TUMIENI ATM KUNUNUA BIDHAA’

NA MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

WATANZANIA wameshauriwa kuendelea kutumia kadi za kielektroniki za benki katika kufanya matumizi ya kila siku na kupunguza kutembea na fedha taslimu ili kupunguza uhalifu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi, Mkuu wa Kitengo cha Malipo ya Kadi wa Benki ya Barclays, Philbert Casmir, alisema ushirikiano wa benki hiyo na Kampuni ya GSM ni juhudi zao za kupeleka huduma karibu kwa wateja wao na kukuza ushirikiano wao na kampuni nyingine za ndani.

Alisema wateja wa benki hiyo wanaweza kupata punguzo la asilimia 15 katika manunuzi yao katika maduka ya GSM kwa kulipia kidogo na kupunguza gharama za manunuzi ya kila siku.

Alisema ushirikiano wa benki hiyo na GSM ni wa mwaka mmoja, ambao utawapa nafasi wateja wao kutumia nafasi hiyo.

“Ushirikiano huu wa kimkakati ni mfano wa kujitolea kwetu kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wetu kwa kutumia kadi za benki kama ufumbuzi wa haraka kufanya manunuzi ya kila siku katika nyakati hizi ngumu za kiuchumi… wateja wanatafuta njia za kuokoa fedha zaidi kwa kulipa kidogo,” alisema.

Alisema benki hiyo sasa ina wateja 70,000 ambao wanatumia kadi katika manunuzi yao ya kila siku, ambapo mwaka jana Barclays walipata tuzo ya Visa Agile, ambayo inatambuliwa kama benki bora Tanzania, ambayo imepata mafanikio katika utumiaji wa kadi.

Kwa upande wake, Meneja wa Masoko GSM Mall, Cecil Mhina, alisema: “Tunastahili sana juu ya ushirikiano huu, tunaamini kuwapa wateja wetu bidhaa bora na za bei nafuu ambazo zinaendana na maisha yao.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles