27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

WATAKIWA KUTUMIA MIFUGO KUSOMESHA WATOTO

Na Ahmed Makongo

WAFUGAJI katika Halmashauri ya Mji wa Bunda wametakiwa kutumia rasilimali yao ya mifugo kusomesha watoto wao waweze kupata elimu inayostahili itakayowasaidia katika maisha yao ya baadaye.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili alisema wazazi nao watafaidika na elimu hiyo kwa kutunzwa vizuri na watoto hao  wanapokuwa wazee.

Alikuwa akizungumza kwenye uzinduzi wa   uwekaji chapa kwenye ng’ombe katika Halmashauri ya Mji wa Bunda uliofanyika katika Mtaa wa Butakare Kata ya Bunda stoo.

Bupilipili alisema   elimu ndiyo msingi wa maisha  hivyo ni vema na haki kwa wafugaji katumia rasilimali ya mifugo yao na kuivuna kwa kuiuza kwa ajili ya kusomesha watoto wao  waweze kupata elimu bora itakayowasaidia katika maisha yao ya baadaye.

“Ninawahimiza ndugu zangu wafugaji musomesheni watoto wenu kwa kutumia hii mifugo yenu.

“Maana ukisomesha mtoto wako utakuwa umefanya jambo jema   maana hiyo elimu itamsaidia yeye   na wewe mzazi wake katika maisha yao ya baadaye,” alisema.

Alisema  ukitaka kufaidi matunda ya nchi hii ni kusomesha mtoto wako kwa sababu baadaye atakusaidia.

DC aliwaambia wafugaji hao kuwa uwekaji chapa kwenye mifugo yao kuna manufaa mengi sana.

Alitaja manufaa hayo kuwa ni   kudhibiti wizi wa mifugo, kujua idadi ya mifugo iliyoko katika halmashauri hiyo, kufuga kisasa kulingana na maeneo ya malisho na kuweka mikakati madhubuti ya kuihudumia mifugo hiyo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Janeth Mayanja, na aOisa Mifugo katika Halmashauri hiyo, Rick Kaduri, walisema   kabla ya kuanza uwekaji   chapa  ng’ombe, kwanza walitoa elimu kwa wafugaji wote  waweze kufahamu umuhimu wa hatua hiyo.

Ofisa mifugo huyo wa halmashauri ya mji wa Bunda alisema  uwekaji wa chapa kwenye ng’ombe linakwenda na usajili wa mifugo yote iliyoko katika halmashauri ya mji huo.

Nao baadhi ya wafugaji hao walifuraishwa na   uwekaji  chapa kwenye ng’ombe wao.

Walisema  serikali inatambua mchango wa wafugaji katika maendeleo ya nchi  kwa sababu  wamekuwa wakishiriki katika shughuli mbalimbali za kuchangia miradi ya maendeleo katika maeneo yao.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles