30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

VIONGOZI WALIOPEWA DHAMANA WAMEKOSA MAADILI-TAHLISO

NA OSCAR ASSENGA- TANGA

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (TAHLISO), Stanslaus Kadugalize, amesema Watanzania wamefika hapa kutokana na baadhi ya watu waliopewa dhamana na Serikali katika nyadhifa mbalimbali kukosa maadili ya uongozi.

Kagudalize aliyasema hayo jana wakati akizungumza na gazeti hili, ambapo alisema kutokana na hilo kwa makusudi ama kwa bahati mbaya, wamesababisha uzembe ambao umeligharimu Taifa.

Alisema fedha hizo ambazo zimepotea zingeweza kusukuma gurudumu la maendeleo kwa kuhakikisha upatikanaji wa maji, ujenzi wa barabara, utoaji elimu bure hadi chuo kikuu, huduma za afya unafikiwa kwa asilimia kubwa ili kuondosha changamoto hizo.

“Fedha ambazo zimepotea, zingesaidia kuinua maendeleo katika nyanja mbalimbali za kielimu, afya na kiuchumi kwa lengo la kusogeza karibu maendeleo kwa wananchi katika maeneo mbalimbali hususani vijijini,” alisema.

Alisema wao kama jumuiya wanasifu juhudi kubwa inazoonyeshwa na Rais Dk. John Magufuli, kupigania na kuzilinda rasilimali za nchi kwa masilahi ya Taifa.

Alisema tangu aingie madaraka, anakaribia kutimiza miaka miwili lakini ndani ya kipindi hicho, Watanzania wameona mambo mengi makubwa yakifanywa.

Alisema moja kati ya mambo makubwa, ni kupambana na vita dhidi ya dawa za kulevya, kuondoa watumishi hewa serikalini  na vyeti feki.

Alisema suala jingine ambalo alilipigania kwa vitendo, ufisadi na uhujumu uchumi na kufufua Shirika la Ndege Tanzania (ATC) kwa kununua ndege mpya.

“Lakini pia kasi yake imewezesha ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa mabweni ya wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), sanjari na utoaji wa ajira zaidi ya 50,000 kwa vijana wahitimu jambo ambalo litawawezesha kunufaika wao na jamii zao,” alisema.

Aliyekuwa Rais wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Tanga, David Manyilizu, alisema msimamo wa Rais Magufuli kusimamia vitu kwa umakini mkubwa, utaifanya nchi ipige hatua kubwa za maendeleo.

“Katika juhudi hizi, Watanzania tumsaidie kwa kumwombea kiongozi huyu ili afikie malengo yake aliyojiwekea,” alisema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles