Renatha Kipaka, Bukoba
WATAHINIWA 2,677 katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wanatarajia kuanza mtihani wao wa kuhitimu kidato cha nne kesho Novemba 15, mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumapili Novemba 14, 2021 na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Bukoba, Hamid Njovu wakati akizungumza na Waanahabari ofisini kwake.
Amesema, kati watahiniwa hao wavulana ni 1,292 na wasichana ni 1,385 huku vituo vya kufanyia mtihani vikiwa 37.
“Hivi vituo vipo kwa makundi matatu kuna shule za serikali 17, shule za binafsi 13 na wale wa kujitegemea 7, wote wameandaliwa kwa mujibu wa Sheria,” amesema Njovu.
Aidha, amesema kuwa katika idadi hiyo watu wenye ulemavu watakapo fanya mtihani uoni hafifu 2, Viziwi 9, ulemavu wa viungo 4 ambao jumla yao ni 15.