25.6 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

WASTARA AMSHUKURU JPM,ATIMKIA SWEDEN

Na Bethsheba Wambura, Dar es Salaam


Msanii wa filamu nchini ,Wastara Juma maarufu Wastara, ametoa shukrani zake kwa Rais John Magufuli, kwa kujitolea kulipia gharama za matibabu yake yaliyofanyika mwezi mmoja uliopita nchini India alikoenda kufanyiwa upasuaji wa mguu aliokatwa kutokana na kupata ajali miaka kadhaa iliopita.

Wastara amesema milioni 15 alizotoa Rais Magufuli, zimesaidia kwa kiasi kikubwa katika matibabu yake na sasa anaendelea vizuri kwani anaweza kusimama na kutembea bila kutumia magongo ambayo alikuwa akiyatumia hapo awali na kumshukuru kwa upendo wake huo aliounesha.

“Namshukuru Rais Magufuli kwa kunisaidia sasa uzuri wangu umerejea na naweza kusimama kutembea bila msaada wa magongo japo si kwa muda mrefu na afya yangu inaendelea kuimarika siku baada ya siku najua Rais ana majukumu mengi ya kufanya lakini aliamua kunisaidia mimi huu ni upendo wa hali ya juu.

“Lakini kwa namna ya kipekee kabisa ningependa kuwashukuru watanzania wote walijitolea kwa hali na mali kwani michango yao imeniwezesha kurejesha furaha yangu baada ya kupata matibabu niliyoyangojea kwa kipindi kirefu baada ya kuwa na changamoto za kiusafiri na gharama za matibabu,”amesema Wastara.

Aidha, Wastara amekuwa Mtanzania wa pekee kuchaguliwa kuwa Balozi wa Shirika la ASOV AFRICA, linaloundwa na waafrika wanaoishi nchini Sweden linalojihusisha na  kusaidia walemavu, watoto waishio katika mazingira magumu na waathirika wa ndoa za utotoni nafasi aliyoipata alipokwenda nchini humo kucheza filamu mwaka jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles