23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Wastaafu 10,500 PSSSF watakiwa kufanya uhakiki

Anna Potinus – Dar es salaam

Mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma (PSSSF), umetoa wito kwa wastaafu kuhakikisha wanafanya uhakiki mara kwa mara na kuachana na tabia ya kupuza ujumbe wa meseji wanaotumiwa kwa lengo la kuwakumbusha kufanya zoezi hilo ili kuepuka usumbufu mbeleni.

Wito huo umetolewa leo Jumatano Juni 12, na Meneja Kiongozi Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa mfuko huo Eunice Chiume, alipotembelea ofisi za New Habari 2006 (Ltd), ambapo amesema kuwa wastaafu 10,500 kati ya 124,500 hawajafanya uhakiki hadi sasa.

“Wastaafu 10,500 kati ya 124,500 hawajajiakiki hadi leo na hao ndio wanaolalamika kuwa hawajakuta fedha zao, nafikiri hii inatokana na kutokuwa na uelewa au taarifa haziwafikii, na tumeshawaambia watoe taarifa iwapo wameshindwa kuja kutokana na kuwa wagonjwa sisi tutawafuata kwasababu hatuwezi kuwafanyia uhakiki bila kuwaona,” amesema.

“Changamoto nyingine ni ya watu kudharau au wengine wanapata ujumbe wa simu lakini wanasahau halafu baadae wasipoona fedha zao wanakuja juu ndio maana ninapenda wahakiki kabla hatujasimamisha maana tukifanya hivyo ni lawama pia,” amesema.

Aidha amesema kuwa wana uhakika wa kuwapata wastaafu hao kwa kuwa iwapo hawatatokea ndani ya kipindi kilichotangazwa watasimamisha malipo yao na baada ya hapo wasipomuona mtu huyo ndani ya miezi sita ndipo watachukua hatua ya kufuatilia iwapo mtu huyo yupo hai au amekufa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles