24.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Polepole: Viongozi CCM msiwe chanzo cha migogoro

RAYMOND MINJA IRINGA

Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humfrey Polepole, amewataka viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia chama hicho kutokuwa chanzo cha migogoro na majungu badala yake wawe suluhisho kwa kufuata malengo ya chama ambayo ni kusimamia serikali na kuwaletea watanzania Maendeleo.

Ameyasema hayo leo Juni 12 katika semina ya kuwafunda makatibu wa uenzi wa ngazi zote mkoani humo ambapo amesema kuwa chama hicho kimejengwa kwenye misingi bora ya kutumikia wananchi na kuwasikiliza ili kujua shida zao.

“Hii ni CCM mpya chini ya mwenyekiti rais John Magufuli na hana utani anataka kazi tu na wale ambao wanaona wameshindwa watupishe maana unapoacha sumu ndani kuna siku itakudhuru tunapogombana wanaoumia ni watanzania waliotupa dhamana ya kusimamia serikali ”amesema.

Amesema kuwa kwasasa mlango uko wazi na kwamba endapo kuna mtu anaona atashindwa kupelekana na kasi ya chama hicho chini ya rais Magufuli ni vyema akapisha na kuacha wanaojua kufanya kazi.

Pia amewataka viongozi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa huku akimtaka katibu wa itikadi na uenezi mkoani humo, Ramadhani Baraza kuendelea kuwatumikia wananchi vizuri kwa kueleza mambo mazuri yanayofanywa na serikalia ya CCM.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,213FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles