27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Wasiochanjwa wafungiwa ndani Austria

VIENNA, Austria

WATU takribani milioni mbili wamepigwa marufuku ya kutoka nje nchini Austria kwa kuwa hawajapata chanjo ya Corona.

Sababu pekee zitakazokubalika kwa watu hao kuonekana nje ni aidha kwenda kazini au kununua vyakula, ikiwa ni sehemu ya jitihada za nchi hiyo kukabiliana na kasi kubwa ya maambukizi.

Kwa wiki moja pekee, maambukizi yamefikia watu 800 kati ya 100,000, takwimu zinazoifanya Austria kuwa nchi iliyo hatarini zaidi Ulaya.

Tayari Serikali imeshafanikisha uchanjaji kwa asilimia 65 ya raia wake, japo ni kiwango kidogo ukilinganisha na mataifa mengine ya Bara hilo. “Hatutachulia poa, kwa bahati mbaya hii itakuwa ni lazima,” amesema Kansela Alexander Schallenberg.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,451FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles