29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wasimamizi wa uchaguzi wanusurika kifo

NA JANETH MUSHI, ARUSHA

BAADHI ya wasimamizi wa uchaguzi wilayani Meru, Mkoa wa Arusha, wamenusurika kuchomwa moto ndani ya gari lao baada ya kundi la vijana kutilia shaka gari lao wakidhani limebeba kura za wizi.

Tukio hilo lililowashtua wasimamizi hao na kujikuta wakiwa hawana la kufanya mikononi mwa kundi la vijana hao, lilitokea katika Kata ya Embaseni, wilayani hapa juzi, kati ya saa tatu na saa nne asubuhi.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walisema vijana hao walilitilia shaka gari hilo na watu waliokuwamo ndani.

Kutokana na hali hiyo, vijana hao walilifuatilia gari hilo na kusababisha purukushani zilizosababisha askari polisi waliokuwa eneo hilo kuingilia kati na kuwaamuru vjana hao kuondoka.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema vijana hao walitilia shaka gari hilo na kudai kwamba lilikuwa na fedha kwa ajili ya kwenda kuwanunua mawakala wa usimamizi wa kura kwenye vituo.

Akizungumzia tukio hilo, Msimamizi wa Uchaguzi, Jimbo la Meru, Damari Mchome, alikanusha madai ya fedha kugawanywa kwa mawakala na kusema fedha hizo zilikuwa ni malipo ya wasimamizi wa kata hiyo na kwamba hakuna fedha zilizoporwa.

“Msimamizi msaidizi wa Kata ya Embaseni alikuwa ndani ya gari ya kampuni za kitalii ambalo lilikuwa limekodishwa na halmashauri.

“Walipokuwa njiani, walikutana na kundi la vijana waliowazingira na kudai wamebeba fedha za kununua mawaka.

“Msimamizi aliyekuwa na mhasibu wetu waliwaonyesha vijana hao fedha na orodha ya malipo kwa wasimamizi, ndipo walipowaachia baada ya kujiridhisha.

“Kimsingi sisi hatuna jukumu la kuwalipa fedha mawakala wa vyama kama walivyokuwa wanadai vijana hao,” alisema Mchome.

“Pamoja na gari hilo kuwekwa nembo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), vijana hao hawakujali na badala yake walitaka kulichoma moto gari hilo kwa madai kuwa kulikuwa na kura za kughushi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles