29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Wasichana 4,000 kupata elimu ya lishe

Hadija Omary-Lindi

WASICHANA 4,000 kutoka halmashauri za manispaa za Lindi na Nachingwea mkoani Lindi, wanatarajiwa kufikiwa na mradi wa lishe kwa watoto wa kike, unaoendeshwa na  World Association of Girls Guide & Girl Scouts. 

Hayo yameelezwa na Kamishina wa Girls Guide Tanzania Association Mkoa wa Lindi (T.G.G.A),  Agnes Chipanda wakati wa uzinduzi wa kongamano la lishe mwishoni mwa wiki.

Alisema kati ya wasichana watakaonufaika na mradi  huo, wasichana 2700 watatoka Manispaa ya Lindi na 1,500 watatoka wilayani Nachingwea.

Mwenyekiti wa Girls Guide Mkoa wa Lindi, Zuhura Mohammed alisema mradi unafanyika kwa majaribio  katika nchi za Tanzania, Bagladesh, Sri Lanka, Philipins na Madagascar

“Mradi huu unatekelezwa mikoa ya Dar es Salaam,Tanga, Arusha, Lindi, Dodoma na Mara. Hapa Lindi tumeanzia Manispaa ya Lindi Nachingwea matarajio yetu ni kuwafikia wasichana 4,000 ifikapo mwaka 2020,” alisema. 

Alisema moja ya malengo ya mpango huo, ni  kutoa elimu ya lishe kwa watoto wa kike ili waweze kula vizuri, kukua vizuri, kuongeza nguvu kazi ya kitaifa.

Akizindua kongamano hilo, Ofisa Utamaduni Mkoa wa Lindi, Makalage  Shekalage  kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa huo,Rehema Madenge aliwataka viongozi kuweka utaratibu mzuri utakaoweza kupanua wigo wa kuongeza  wasichana hasa walio mtaani ili elimu hiyo iwafikie.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles