24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Washtakiwa 40 wa Mfalme Zumaridi wapewa dhamana

Na Clara Matimo, Mwanza

Washtakiwa 40 kati ya 85 wa kesi namba 12/2022 inayomkabili Diana Bundala maarufu kama ‘Mfalme Zumaridi’ na wafuasi wake wameachiwa  kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza leo Machi 9, 2022.

Ikumbukwe kwamba Machi tatu mwaka huu washtakiwa hao pamoja na Mfalme Zumaridi walifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza  na baada ya kusomewa mashtaka yao  mbele ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Monica Ndyekubora, ambapo walipewa dhamana walikataa wakisema kwamba hawawezi kumuacha kiongozi wao hivyo nao walipelekwa rumande.

Washtakiwa hao walisomewa  mashtaka matatu ambayo ni kuzuia maofisa wa Serikali kutekeleza majukumu yao, kufanya mkusanyiko usiyo na kibali na shtaka la usafirishaji haramu wa binadamu lililokuwa likimkabili Mfalme Zumaridi peke yake ambalo ni jinai isiyo na dhamana.

Wakili wa washtakiwa hao, Erick Mutta, amewaambia waandishi wa habari leo baada ya washtrakiwa hao kupewa dhamana, kwamba “Dhamana imetolewa baada ya mshtakiwa namba moja wa shauri hilo (Mfalme Zumaridi) kuiomba mahakama kuwaachia kwa dhamana washtakiwa wanaoweza kudhaminika katika kesi hiyo.

“Baada ya kuwasilisha ombi hilo washtakiwa 40 ndiyo wamekubali kudhaminiwa 45 wamekataa dhamana  wakiomba waendelee kusota rumande na kiongozi wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles