28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania kufaidika zaidi utunzaji rasilimali maji

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi amesema Tanzania inaendelea kunufaika pamoja na wananchi wake kwa kujenga uhusiano mzuri na mataifa mbalimbali zikiwemo nchi jirani zinazoizunguka.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete akipokea tuzo mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kwanza wa Baraza la Mawaziri, Kamisheni ya Bonde la mto Songwe uliofanyika jijini Lilongwe, Malawi.

Amesema hayo wakati wa mkutano wa kwanza wa Baraza la Mawaziri, Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe uliofanyika jijini Lilongwe, Malawi.

Amesema kupitia Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe kazi inafanyika kwa ushirikiano kuondosha changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Tanzania na Malawi kupitia wataalamu wa rasilimali za maji, ikiwemo ujenzi wa mabwawa katika bonde hilo ambayo itakuwa suluhu ya mafuriko yanayoharibu mali mbalimbali ikiwamo mazao kwa kujenga bwawa la Songwe Chini na mazingira.

Aidha kuwezesha kilimo cha umwagiliaji zaidi ya hekta 6,000 na kupata nishati ya uhakika ya umeme kwa nchi mbili kugawana megawati zipatazo 180.

Amesema hayo ni mafanikio ya mahusiano yaliyojengwa na viongozi wa nchi mbili katika kuhakikisha wananchi wanafanya kazi kwa maendeleo ya nchi zao.

“Kazi hii ni matunda ya viongozi wetu mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na mheshimiwa Lazarus Chakwera, Rais wa Malawi,” amesema Mahundi.

Amewataka wananchi kuendelea kutunza mazingira na vyanzo vya maji ili kuhakikisha huduma ya maji na miradi ya maji inakuwa endelevu na kutosheleza mahitaji ya jamii kwa sasa na vizazi vijavyo.

Kamisheni ya Bonde la mto Songwe inaundwa kwa pamoja na nchi za Malawi na Tanzania ambapo katika kikao hicho mawaziri wamekubaliana na kusaini kanuni za uendeshaji wa vikao vya mawaziri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles