27.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Wasanii watunukiwa tuzo Siku ya Msanii

JANGALANA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

WASANII wanne wa sanaa mbalimbali nchini juzi wametunukiwa tuzo maalumu katika usiku wa tuzo za wasanii zilizofanyika katika ukumbi wa Nyumba ya Sanaa, Posta Dar es Salaam.

Tuzo hizo zilitolewa na Katibu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Michezo na Wasanii, Elisante Gabriel, huku ikihudhuriwa na wasanii mbalimbali.

Tuzo ya kwanza ya heshima ya sanaa za maonyesho ilikwenda kwa mwigizaji mkongwe nchini ambaye michezo yake ilikuwa ikisikika kwenye redio Tanzania enzi hizo, Bakari Mbelembe ‘Mzee Jangala’.

Tuzo ya sanaa ya ufundi ilikwenda kwa Robert Yakobo ‘Sangwani’ huku tuzo ya heshima katika filamu akitunukiwa Thecla Mjata na Tuzo ya heshima katika muziki ilikwenda kwa mwimbaji mkongwe wa muziki wa mwambao, Shakira Said ‘Bi Shakira’.

Akizungumza kabla ya kukabidhi tuzo hizo, Katibu huyo alisema ufike wakati wasanii watambue thamani yao na sio kujirahisisha kitendo kinachowafanya kuonekana ni rahisi.

“Nyie mna thamani kubwa sana, msijirahisishe kwa kufanya kazi za bei rahisi ambazo haziendani na thamani yenu mtakuwa hamjitendei haki na kuzidi kushusha thamani ya sanaa nchini.

“Serikali imetambua mchango na umuhimu wenu na ndiyo maana kuna mabadiliko makubwa yaliyofanywa kwenye wizara hii kwa kuwekwa wasanii kitu ambacho hakikuwepo, sasa tunataka kuona nanyi mnalitendea haki Taifa, nidhamu ni jambo la msingi na linapaswa kufuatwa lakini pia masuala yenu muyamalize wenyewe sio kitu kidogo mnakimbilia vyombo vya habari, mnajiharibia sifa,” alisema Gabriel.

Usiku huo ulipambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa kundi la ngoma za asili na sarakasi la Dar Creative, Msanii wa kuigiza sauti za wasanii mbalimbali na watu maarufu, Mlugaluga pamoja na bendi ya K-Mondo Sound.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles