BAADA ya Kanye West na mke wake Kim Kardashian, kufanikiwa kupata mtoto wa kiume ambaye amepewa jina la Saint West, msanii ameamua kuumiza kichwa kwa ajili ya kumpa zawadi ya wimbo mtoto huyo.
Kwa sasa mtoto huyo amekuwa akitajwa sana katika mitandao ya kijamii kutokana na umaarufu wa baba na mama yake, lakini Kanye West amesema anatarajia kuachia wimbo mkali ambao utakuwa ni zawadi kwa mtoto huyo.
“Mungu ametupatia zawaidi ya mtoto mwingine, lakini na mimi ninataka kumpa zawadi ya wimbo mtoto huyo, nina nyimbo nyingi lakini hadi sasa sijui nimpe zawadi ya wimbo gani,” alisema Kanye West.
Mtoto wao wa kwanza wa kike walimpa jina la North West, alizaliwa Juni 2013, hivyo watu walidhani kuwa mtoto huyu wa sasa watampa jina la South au East.
Kim amesema wamempa mtoto wao jina la Saint kwa kuwa aliteseka sana wakati wa mimba yake na ndio maana wamempa jina la hilo likiwa na maana ya ‘Mtakatifu’.