Wasanii wanogesha KiliFest 2015

0
620

kilifest Navy KenzoNA MWANDISHI WETU

TAMASHA la KiliFest limefanyika kwa mara ya kwanza katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam, huku wasanii wa muziki wa aina mbalimbali wakinogesha tamasha hilo.

Wasanii waliopanda jukwaani na kunogesha tamasha hilo kwa shoo zao kali ni Isha Mashauzi, Mapacha Watatu, Maua, Ruby, Damian Soul, Navy Kenzo, Fid Q, Ben Paul, Vanessa Mdee, Shettah na kundi la Weusi.

Tamasha hilo lilidumu takribani saa 18 baada ya kuanza saa nne asubuhi na kumalizika saa tisa na nusu usiku.

Licha ya wasanii wote hao kufanya onyesho bora, lakini pia michezo mbalimbali ilifanyika katika viwanja hivyo huku washindi wakipata fursa ya kujumuika na mastaa mbalimbali.

“Tulidhamiria kufanya kitu kizuri, watu wamepokea tamasha hili ambalo tutaliendeleza miaka ijayo ili wateja wetu na wapenzi wa burudani wapate kitu tofauti na cha aina yake,” Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here