26.9 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Wasanii, wadau wa Sanaa wakutana kujadili changamoto zinazowakwamisha

Na Grace Mwakalinga, Mtanzania Digital

WASANII kutoka kada mbalimbali, wadau wa sekta ya Sanaa wamekutana jijini Dodoma kujadili vikwazo wanavyokabiliana navyo wakati wa kutekeleza majukumu yao..

Kikao hicho ambacho kimefanyika leo jijini humo kimewahusisha wadau kama vile Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) na Taasisi ya Hakimiliki (COSOTA) ili kupata suluhu ya masuala yanayohusu haki na maslahi ya wasanii Tanzania.

Agness Kahamba, msanii wa maigizo nchini amesema wanapitia changamoto nyingi wakati wa kutekeleza majukumu yao na kwamba vinapoandaliwa vikao kama hivyo vinatoa fursa kueleza wanayoyapitia kwa ajili ya kupata suluhu kwa wadau wao.

“Tunatamani kufanya Sanaa yetu kibishara kwa kuuza bidhaa tunazozizalisha ndani na nje ya nchi lakini changamoto ni maslahi duni na kukosa mitaji ya kuandaa kazi bora zenye ushindani. Tunaimani Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kupitia ziara alizozifanya mataifa mbalimbali zinaendelea kutangaza sanaa zetu,” amesema Agness.

Mkuu wa Idara ya Sheria wa Kituo cha Kutetea Haki za Wasanii Tanzania (TARO), Ally Ramadhan, amesema wameendesha vikao mbalimbali kuhusu wasanii kupokea mapendekezo yao.

Amesema baada ya mapendekezo hayo Taro watayachakata na hapo baadae watayapeleka bungeni kwa ajili kufanyiwa maboresha na kutungwa kwa sheria zitazoendelea kuwalinda wasanii nchini.

Kwa upande wake wakili wa Baraza la Sanaa la Taifa, Joseph Ndosi, amesema wao kama walezi wa sekta ya Sanaa wataendelea kuwashauri wasanii namna bora ya kuzalisha kazi zenye ushindani ili kufikia malengo waliyokusudia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles