22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Wasanii nchini wanavyonufaika na Tigo Music

bellaNA MWANDISHI WETU

LICHA ya changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya muziki nchini, sekta hiyo imeendelea kuwa mkombozi kwa vijana hasa kupitia muziki wa kizazi kipya.

Muziki huo umewatengenezea ajira vijana wengi wenye vipaji vya muziki kiasi kwamba umeleta sifa kubwa nchi za Afrika Mashariki, Afrika kwa ujumla na hata Ulaya.

Lakini licha ya muziki huo kuendelea kuwa na mafanikio kwa baadhi ya wasanii, wengi wao bado hawajui sheria za hati miliki za kazi zao za kimuziki pamoja na mambo mengine ya kisheria.

Tigo Tanzania ni moja ya makampuni ya kidijitali iliyoanzisha jumuiya ya wanamuziki wa kizazi kipya ijulikanayo kama ‘Tigo Music Platform’ yenye lengo la kuwawezesha wasanii wa muziki nchini wajulikane wao na kazi zao za muziki ndani na nje ya nchi.

Mradi wa Music Platform uliozinduliwa nchini Januari 2015, hadi sasa umeshawezesha wanamuziki wa Tanzania wapatao 20.

Meneja wa mradi huo, Balla Shareeph, anasema mradi huo umesaidia muziki wa Tanzania na wasanii wake kujulikana kimataifa kupitia mfumo wa kusambaza nyimbo zao kwa njia ya mtandao wa kimataifa ujulikanao kama ‘streaming’.

“Kupitia mradi huu wasanii wa Tanzania wamepata fursa ya kujulikana kimataifa, vile vile wamepata fedha za ziada kutokana na nyimbo zao jambo ambalo ndiyo lengo kuu la kuanzisha mtandao huo unaowaunganisha wasanii na mashabiki wao,” anaeleza Shareeph.

Shareeph anafafanua zaidi kwamba mradi huo pia unatoa mafunzo kwa wanamuziki na inawajengea uwezo wasanii wanaochipukia ili waongeze ujuzi na kujenga maisha yao kuwa bora zaidi.

“Mtandao wa kusambaza muziki duniani kote unakuwa kwa haraka, vile vile ni wa pili kujulikana kama mtandao wa simu Kusini mwa bara la Afrika,” anaongeza.

Pia Shareeph anasema kwamba kampuni ya Tigo imekuwa ikiwatia moyo wanamuziki wa ndani kuwa karibu na shirika la haki za muziki barani Afrika, yaani Africa Music Right ambao huwadhamini na kupandisha chati haki za muziki barani Afrika ili wanamuziki waweze kutawala soko la muziki Afrika.

Kwa sasa Tigo Tanzania imekuwa karibu na kampuni ya kimataifa ya Kifaransa ambayo kazi yake kubwa ni kusambaza muziki duniani ikijulikana kama Music Streamer Deezer.

Tigo husambaza na kupata miziki zaidi kote duniani kupitia simu za mkononi, ambapo inatoa njia milioni 36 za kusambaza miziki mbalimbali duniani.

Wasanii wanaonufaika

Baadhi ya wasanii wanaonufaika na mradi huo ni Young Dee na Christian Bella ambao kila mmoja alichangia kwa mtazamo wake kuhusiana na mradi huo.

Young Dee

Msanii David Genz maarufu kama Young Dee, anasema amenufaika na nyanja zote za kitaifa na kimataifa.

“Mradi huu ni ukombozi kwa wanamuziki wachanga, mimi umeniwezesha kujulikana kimataifa, naishukuru kampuni ya Tigo Tanzania kwa kusaidia wasanii kama mimi,” anaeleza Young Dee.

Christian Bella

Mwanamuziki mwingine anayenufaika na mradi huo ambaye ni raia wa Congo anayeishi jijini Dar es Salaam, Christian Bella, anapongeza mradi huo kufanyika kwa ubunifu unaowezesha wanamuziki wa Tanzania kunufaika.

“Naheshimu tigo kwa kupandisha chati miziki ya wasanii hapa Tanzania jambo ambalo linakuza fani ya muziki na wasanii kwa ujumla,” anasema Bella.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles