26.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Wasaidizi kisheria waaswa

NA ALLY BADI, LINDI
OFISA Mfawidhi Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Kanda ya Kusini, Mourice Chisi, amewataka wasaidizi wa kisheria kutumia nafasi zao kuwasaidia wananchi mkoani hapa kutatua migogoro bila upendeleo.
Wito huo ameutoa wakati alipokuwa anafunga kikao kazi na kugawa vyeti kwa wahitimu wasaidizi wa kisheria kutoka wilaya sita za Mkoa wa Lindi kilichoandaliwa na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake na Watoto Mkoa wa Lindi (LIWOPAC).
Alisema wasaidizi wa kisheria ni watu muhimu maeneo ya vijiji ambako huduma za mahakama ziko mbali.
“Nichukue nafsi hii kuwaomba wasaidizi wa kisheria kuwa waadilifu na kuwasaidia wananchi wanaokabiliwa na migogoro mbalimbali, hasa utetezi wa haki za wanawake, watoto na jamii kwa ujumla,” alisema Chisi.
Kwa upande wake, Mratibu wa LIWOPAC, Cosma Bulu, alisema kikao hicho ni cha kazi kwa wasaidizi wa kisheria cha kujadili changamoto na mafanikio yaliyopatikana katika utendaji kazi na kubadilishana uzoefu.
Alisema kwa kipindi cha mwaka 2013/14, wasaidizi wa kisheria wameweza kufanya kazi mbalimbali ikiwamo kutatua migogoro ya kijamii na kupunguza wananchi kupeleka kesi mahakamani kudai haki zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles