30.3 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Wasafirishaji nchini wahimizwa kutii sheria kwa kubeba uzito stahiki

Na Mwandishi Wetu,Mtanzania Digital

WASAFIRISHAJI nchini wamehimizwa kutii sheria kwa kubeba uzito unaotarajiwa ili kulinda barabara.

Wito huo umetolewa jana Dar es Salaam na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Rogatus Mativila wakati akifungua mafunzo ya utoaji elimu kwa wasafirihaji juu ya upimaji uzito wa magari kwa kutumia Sheria ya Afrika Mashariki ya kudhibiti uzito ya mwaka 2016.

MSIMAMIZI wa Mizani kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi , Mhandisi Leonard Saukwa, akitoa elimu kwa wadau wa sekta ya usafirishaji, juu ya sheria ya Afrika Mashariki ya udhibiti wa uzito wa magari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018, jana Dar es Salaam.

Mhandisi Mativila alisema mafunzo hayo yanalenga kutoa uelewa wa sheria ya udhibiti uzito wa magari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 na kwamba jukwaa hilo litatumika kupokea maoni, ushari na namna ya kuendelea kuboresha utendaji kazi.

“Niwaase wasafiridhaji wote kutii sheria katika utendaji wa kazi zenu pia niombe watendaji wetu kutoa huduma kwa wakati kwa kuzingatia sheria, kwa umoja wenu muendelee  kutunza barabara zetu kwa kubeba uzito unaokubalika,” alisema Mhandisi Mativila.

Aidha ameongeza kuwa ni imani ya serikali kuwa baada ya mafunzo hayo makosa ya kuzidisha uzito katika barabara yatapungua.

WADAU wa sekta ya usafirishaji, wakifuatilia mafunzo juu ya sheria ya Afrika Mashariki ya udhibiti wa uzito wa magari.

“Inategemewa kuwa baada ya mafunzo haya makosa ya kuzidisha uzito katika barabara zetu yatapungua,hivyo tutaendelea kuzitunza ili ziweze kuleta tija,ikumbukwe kwamba Serikali inatumia fedha nyingi sana katika kujenga barabara ili ninyi wasafirishaji muweze kuzitumia kusafirisha mizigo mbalimbali na kuchangia uchumi wa nchi kwani tunategemeana.

“Hivyo, kunapokuwa hakuna barabara, hakuna usafirishaji, hivyo ni vema mtambue kwamba hivi vitu ni vyenu, elimu hii inatolewa ili muielewe siyo suala la kukwepa kwepa,” alisema Mhandisi Mativila

“Ni suala la kutambua kuwa barabara hiyo utakapo ipondaponda basi na wewe shughuli yako itakufa, niwakumbueshe kuwa serikali ipo mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa wananchi wake wanapata huduma bora, hivyo iwapo barabara hazikuwa bora hazitapatikana,”alisema.

Msimamizi wa Mizani kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Leonard Saukwa  alisema semina hiyo imelenga  kuwajengea uwezo wasafirishaji na wamiliki wa magari ya mizigo ili  kuelewa sheria ya udhibiti  uzito ya Afrika Mashariki na kanuni zake na kwamba watazunguka nchi nzima katika vituo 13 kwa ajili ya kutoa elimu hiyo.

“Tutazunguka nchi nzima kwa ajili ya kutoa mafunzo ili kuwaelimisha wasafirishaji na wamiliki wa vyombo vingine ikiwamo mabasi, kwani kumekuwa na malalamiko ambayo yamekuwa yakitufikia wizarani kwamba tozo zimekuwa zikibadilika mara kwa mara na hawafahamu ni kwa namna gani wanatozwa.

“Hivyo, kutokana na hilo ndiyo maana tukaja na mkakati huu ili kwanza kuwasaidia kufanhamu sheria hiyo ya Afrika Mashariki ili waelewe namna ya kulinda barabara zetu na hicho ndicho tunachokifanya, kama wizara kwa kuwa ni wajibu wetu,” alisema Mhandisi Saukwa.

Mafunzo hayo ambayo yanashirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya usafirishaji yamepangwa kufanyika katika Mikoa 13 ikiwemo  Dar es Salaam,Mtwara, Morogoro,Dodoma,Njombe,Mbeya, Rukwa, Ruvuma, Kigoma,Geita, Tabora, Mwanza, Arusha na Tanga.

Sheria hiyo inatumika kwenye nchi zote za Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles