24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

UDSM yaipongeza Serikali kwa kudhibiti Uviko-19

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM) umeipongeza Serikali kwa hatua ilizochukua na inazoendelea kuchukua katika kukabiliana na ugonjwa wa corona unaotishia maisha ya watu na uchumi wa nchi.

Akizungumza katika mahafali ya 51 ya chuo kikuu cha Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema serikali kupitia Wizara ya Afya imeonesha juhudi za kupambana na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kutoa miongozo.

“Serikali kupitia wizara ya afya imejitahidi kupambana na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kutoa miongozo mbalimbali kwa watanzania juu ya namna ya kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi ya UVIKO 19,” amesema Jaji Lubuva.

Amesema wahitimu wanawajibu wa kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kujikinga na maambukizi ya UVIKO 19 ili kusiweze kupotea kwa nguvu kazi ya taifa.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa William Anangisye amesema changamoto ya UVIKO 19 imeendelea kuathiri shughuli za chuo kama vile makongamano, utafiti na pia idadi kubwa ya wanafunzi wa kigeni hawajaweza kurudi chuoni kuendelea na masomo kutokana na athari za ugonjwa huo.

Aidha, ameishukuru serikali kwa kuendelea kukiwezesha chuo ikiwemo kukipatia fedha za kuendesha shughuli mbalimbali huku akimuhakikishia mkuu wa chuo hicho Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ya kwamba fedha zote chuo inazopewa na serikali zitatumika kwa matumizi ya chuo na endapo itadhihirika fedha hizo kutumika kinyume na matarajio, baraza la chuo halitosita kuwachukulia hatua kali wahusika kwani ni kinyume na sheria

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles