27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wasafi Festival yaacha historia Dar

CHRISTOPHER MSEKENA

MAELFU ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, juzi walijitokeza kushuhudia burudani ya kukata na shoka kwenye kilele cha tamasha la Wasafi ‘Wasafi Festival’ lililofanyika viwanja vya Posta Kijitonyama.

Tamasha hilo ambalo limefanyika kwa mara ya kwanza jijini Dar es salaam, limekonga nyoyo za mashabiki wa aina zote za muziki kama vile Dansi, Taarabu, Singeli, Injili, Bongo Fleva ya sasa na zamani pamoja na mastaa kadhaa kutoka nje ya nchi.

Mwenyeji wa Wasafi Festival, Diamond Platnumz  aliandika historia kwa kupiga shoo pendwa iliyojaa ubunifu na kuwafanya mashabiki waimbe naye mwanzo mwisho huku Wizkid, Tiwa Savage, Innos B kutoka Kongo na Meddy wa Rwanda nao walionyesha maajabu yao.

Awali mashabiki walifika mapema kwenye viwanja hivyo na kuanza kupata burudani ya muziki wa Dansi, Taarabu na Singeli kutoka bendi za Twanga Pepeta, Bogoss Musica chini ya Nyoshi El Sadaat, Malkia wa mipasho, Khadija Kopa, Mzee wa Bwax, Sholo Mwamba na Dullah Makabila.

Pia wakali wa kama Jux, Young Killer, Amber Lulu, Gigy Money, Lavalava, Mbosso, Rayvanny,  Orbit Makaveli na Chin Bees waliwakilisha vyema kizazi cha sasa.

Hali kadharika jukwaa hilo lilipambwa na wakongwe wa Bongo Fleva kama vile Ferooz, Z Anto, Pingu na Deso, Profesa Jay, Juma Nature, Chid Benzi, Madee, Queen Darleen, TMK Family, Tip Top Connection, Nyandu Toz, Mandojo na Domo Kaya, Dudu Baya na T.I.D.

Akizungumza na maelfu ya mashabiki uwanjani hapo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alisema onyesho hilo ambalo lilitakiwa kuisha saa sita usiku liendelee hadi saa 11 alfajiri sababu asilimia 20 ya mapato yatakwenda kusaidia watoto wanaosumbuliwa na moyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili huku akionyesha shauku ya kuona ushindani wa matamasha unakuwepo.

 “Mwakani nataka kugawa Dar es Salaam vipande vitatu kiburudani, nataka kipande kimoja Muziki Mnene, kipande cha pili Fiesta na kipande cha tatu Wasafi Festival harafu nione nani ni baba lao na tunampa tuzo mwaka 2020,” alisema Makonda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles