Chris Brown apiga mnada nguo zake

0
887

LOS ANGELES, MAREKANI

STAA wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, mwishoni mwa wiki iliopita alipiga mnada nguo zake zilizokuwa kwenye nyumba huko jijini Los Angeles.

Mapema wiki iliopita msanii huyo alitumia ukurasa wake wa Instagram na kuweka wazi kuwa, wapo mashabiki ambao wanatamani kuwa na nguo zilizovaliwa na msanii huyo, hivyo aliona bora atangaze kuzipiga mnada ili mashabiki watimize ndoto zao.

Baada ya msanii huyo kutoa tangazo hilo, mashabiki walijitokeza kwa wingi huku wengine wakiwa walanguzi kwa ajili ya kununua kwa bei ya chini na wao kwenda kuziuza kwa bei ya juu.

“Nilikuwa mmoja kati ya mashabiki wa Chris Brown, siku zote nimekuwa nikivaa nguo aina ya zile ambazo yeye anazivaa, lakini furaha yangu kubwa ni kuona ninavaa moja kwa moja nguo yake,” alisema mmoja wa mashabiki wa msanii huyo ambae alinunua baadhi ya nguo zake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here