Kiungo Azam atamba sasa wanaanza kazi

0
520

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KIUNGO wa Azam FC, Frank Domayo, amesema wanaamini wataendeleza ushindani katika mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara na kupata matokeo mazuri yatakayowaweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi.

Azam katika mchezo wao wa mwisho walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Biashara United, kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Domayo alisema kwa sasa wanaelewana vizuri hali inayowafanya wazidi kuongeza morali ya kupambana na kupata matokeo.

“Kuna baadhi ya makosa yamejitokeza kwenye huu mchezo lakini hata hivyo kocha wetu atayafanyia kazi baadhi ya mapungufu ili yasijitokeze katika mechi nyingine,” alisema.

Alisema baada ya ushindi huo umezidi kuwatia nguvu ya kuzidisha umakini katika mechi ambazo zinawakabili mbele yao ili wapate matokeo mazuri na kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi.

Domayo aliwataka mashabiki waendelee kuwapa sapoti ili wafanye vizuri na kuendelea kuleta ushindani katika ligi ili watimize mipango yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here