Na Ashura Kazinja – Morogoro
WARATIBU wa ugonjwa wa Ukimwi wametakiwa kuuelewa vyema na kuwa mabalozi wa kuusambaza mkakati wa nne wa taifa wa kudhibiti ugonjwa huo ili kutimiza lengo la kupunguza maambukizi mapya kwa zaidi ya asilimia 85 ifikapo mwaka 2023.
Wito huo umetolewa jana mkoani hapa na Katibu Tawala Msaidizi, Ernest Mkongo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa usambazaji wa mkakati huowa mwaka 2018-2022/23, ulioratibiwa na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) kwa waratibu hao.
Alisema uandishi wa mkakati huo umezingatia dhana ya ushirikishwaji kwa ngazi zote kutoka sekta mbalimbali, zikiwamo asasi za dini, sekta binafsi na wadauwa maendeleo na jamii kwa ujumla ili kuona namna ya kufanikisha dhamira yakufikia ‘Tanzania bila Ukimwi’ na malengo ya dunia ya sifuri tatu ifikapo mwaka2030.
“Tanzania kama nchi nyingine ulimwenguni imeridhia naina endelea kutekeleza malengo na shabaha za kimataifa za kufikia sifuri tatu ifikapo mwaka 2030, kwa maana ya sifuri ya maambukizo mapya, sifuri ya vifovitokanavyo na VVU na Ukimwi, na sifuri ya unyanyapaa na ubaguzi kwa WAVIU,”alisema.
Alisema pia kuhakikisha uwapo wa huduma bora na zenyekiwango cha juu katika ngazi zote na kuweka mazingira wezeshi yatakayocmwongozakila mwananchi katika mapambano dhidi ya Ukimwi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TACAIDS, Jumanne Isango alisemamkakati huo umeainisha vipaumbele mbalimbali, ikiwamo kuhakikisha wananchi wanajua afya zao kwa kusisitiza upimaji wa hiari wa VVU.
Alisema takwimu zinaonesha asilimia 52 tu ya Watanzania ambao wanaishi na virusi vya Ukimwi wanajitambua, huku lengo likiwa ni kufikia asilimia 90 ya watu wanaoishi na virusi kujitambua.
Isango alisema eneo jingine linalotakiwa kushughulikiwa ni kuwa na dawa za kutosha za kupunguza makali ya VVU (ARV’s), na kuhakikisha asilimia90 ya wananchi watakao jitambua wanaanza mara moja kutumia dawa hizo.
“Tumeweka kipaumbele katika swala zima la kupima, na kuweka ubunifu wa kuwa na utaratibu wa wananchi kupata urahisi wa kupima. Mfano kwenye maeneo ya wazi, vituo vya afya na maeneo ambayo si rahisi kufikika kama maeneo ya kazi yenye mazingira hatarishi mfano ya migodini na wavuvi,” alisema.