30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 9, 2021

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

Na Upendo Mosha-Moshi

MKUU wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Kippi Warioba, ametuhumiwa na wananchiwa Kijiji cha Chekereni Weruweru, Kata ya Kindi kuvamia na kuvunja ofisi ya kijijihicho na kuchukua nyaraka mbalimbali.

Kutokanana hali hiyo wananchi hao wametishia kumfikisha mahakamani kwa madai ya kuvunja kufuli la ofisi ya kijiji na kuchukua nyaraka hizo.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, John Bosco, aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana kijijini hapo.

Bosco alisema kiongozi huyo amekuwa ni sehemu ya kuchochea migogoro na kwamba hawapotayari kuchonganishwa bali watafuata sheria.

Alisema mgogoro huo ulianza baada ya mkuu huyo wa wilaya, kutumia nguvu nakuwanyang’anya kijiji ofisi yake na kukipa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jambo ambalo ndio chanzo cha mgogoro huo.

“Tunataka mahakama itafsiri kuwa ofisi ya Kijiji cha Chekereni Weruweru ni mali ya Serikaliya kijiji au CCM… mkuu wa wilaya ametumia vigezo gani kuhalalisha kuwailikuwa mali ya chama hicho na kudiriki kuja kuvunja ofisi  yetu. Tulitegemea yeye ndio atatue migogoro,lakini amekuwa sehemu ya kuichochea,” alisema.

Mjumbe wa Serikali ya kijiji hicho, Omari Omari, alisema ofisi hiyo walikabidhiwa Februari 2, 2015 na Serikali ya kijiji iliyotangulia baada ya uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2014.

“Ofisihii ni mali ya kijiji, tulikabidhiwa jengo, nyaraka na eneo la kijiji hekta 42,175, hakuna mahali imeandikwa hii ni ofisi ya CCM, tumeitumia kwa miaka yotetangu izinduliwe mwaka 1993 na aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu, Agustino LyatongaMrema,” alisema.

Alisema kutokana na kuporwa kwa ofisi hiyo, kijiji kimekodisha jengo jingine kwashughuli za mwenyekiti huku halmashauri ya wilaya nayo ikikodisha jengo tofautikwa ofisi ya mtendaji wa kijiji.

Baadhi ya wananchi, Omary Saidi, Haji Mkumbwa na Elizabeth Gunda walisema mkutano wa kijijiwa Agosti 3, mwaka huu uliazimia jengo hilo lisikabidhiwe kwa CCM kwani si maliyao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Tatu Selemani, alikiri kuwepo kwa tukio hilo, lakini alitaka mkuu wa wilaya aulizwe kwani ndiye aliyetoa maelekezo.

Naye DC Warioba alipohojiwa kuhusu tukio hilo, alisema hawezi kulizungumzia bali anamambo mengi yanayohusu maendeleo ya wananchi.

“Siwezi kulizungumzia jambo hilo, nina mambo ya kufanya na yanahitaji ‘deadline’,lakini kaulize vizuri ile ilikuwa ofisi ya TANU na baadaye CCM, mimi nimewakabidhi wenye mali, hilo si jambo la maendeleo,” alisema.

Hata hivyo kwa mujibu wa maelekezo ya aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Leonidas Gama katika ziara yake ya Februari 19 na 20, 2015 alielekeza kutenganishwa mali na ofisi za Serikali za vijiji na zile zinazomilikiwa na vyama vya siasa.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,702FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles