26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

WAPINZANI WASUSIA HAFLA KUAPISHWA RAIS MNANGAGWA

 

HARARE, Zimbabwe


VIONGOZI  wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini hapa, MDC Alliance, wamesusia hafla ya kuapishwa rasmi Rais Emmerson Mnangagwa, kuwa kiongozi wa nchi hii.

Hafla hiyo ilifanyika jana mjini hapa na kuhudhuriwa na maelfu ya wafuasi wengi wa chama tawala cha Zanu-PF ambacho kiliundwa na Rais Robert Mugabe.

Hata hivyo, pamoja na hafla hiyo kususiwa na wapinzani, jambo hilo lilionekana kutowasumbua wafuasi wa  Rais Mnangagwa, ambao walijitokeza tangu mapema kuandamana kuingia uwanjani huku wakiimba nyimbo za kumsifu kiongozi huyo.

Pia hali ya ulinzi ilionekana kuwa ya hali ya juu isivyo kawaida nje na ndani ya uwanja, huku kila mmoja aliyekuwa akiingia akikaguliwa.

Hafla ya kuapishwa kiongozi huyo imekuja ikiwa ni siku moja tangu Mahakama ya Katiba kukataa pingamizi iliyowekwa na wapinzani wakipinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliompa ushindi.

Katika kesi hiyo  Chamisa‚ ambaye ni alikuwa akipinga  matokeo hayo ambayo yalimpa asilimia 50.8 ya ushindi Rais Mnangagwa huku yeye akiambulia asilimia 44.5  haukuwa huru akidai kwamba  kulikuwapo na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Rais Mnangagwa alikula kiapo hicho mbele ya Jaji Mkuu,  Luke Malaba, ambaye alikuwa miongoni mwa jopo la majaji ambao walitupilia mbali madai ya kiongozi wa Chama cha  MDC, Nelson Chamisa, anayedai aliibiwa kura.

Katika hotuba yake aliyoitoa mara baada ya kuapishwa Rais Mnangagwa, aliahidi kushirikiana na wapinzani ili kuhakikisha Zimbabwe inaimarika zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles