24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

SENETA WA MUDA MREFU MAREKANI AFARIKI

 

WASHINGTON DC, Marekani


SENETA John McCain ambaye alikuwa  shujaa wa vita ya Vietnam na aliyedumu kwa muda mrefu kama seneta nchini  hapa na ambaye pia aliwahi kuwania kiti cha urais, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81.

Habari zilizopatikana jana mjini hapa kutoka katika ofisi yake, Seneta McCain, ambaye jina lake kamili ni John Sidney McCain III, alifariki dunia juzi  akiwa amezungukwa na jamaa zake, baada ya mwaka jana  kugundulika  kuwa na saratani hatari ya ubongo iliyokuwa inasababisha uvimbe kwenye ubongo wake.

Taarifa ya familia yake ilieleza kwamba, seneta huyo ambaye aliondoka mjini hada Desemba mwaka jana na kuacha majukumu yake ili kwenda kupatiwa matibabu, aliamua kuacha kupokea tiba  Ijumaa kabla ya kesho yake kufariki.

Kwa mujibu wa binti yake, Meghan, jukumu kuu alilonalo sasa maishani mwake litakuwa ni kuishi kwa mfano wa baba yake, kutimiza matarajio yake na kufikia kiwango chake cha upendo.

“Siku na miaka ijayo haitakuwa vile tena bila baba yangu, lakini zitakuwa siku njema, zilizojaa uhai na upendo, kwa sababu ya mfano mwema aliokuwa maishani mwake,” aliandika binti huyo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter.

Seneta huyo aliyehudumu bungeni kwa mihula sita, aliwania urais mwaka 2008 kupitia Chama cha Republican, lakini akashindwa na mgombea wa Chama cha Democratic, Barrack Obama.

Madaktari waligundua alikuwa anaugua saratani ya ubongo walipokuwa wanamfanyia upasuaji kuondoa damu iliyokuwa imeganda kichwani juu ya jicho lake la kushoto Julai mwaka jana.

McCain alikuwa mwana na mjukuu wa maofisa wakuu katika Jeshi la Wanamaji nchini  hapa na alikuwa rubani wa ndege za kivita wakati wa vita ya Vietnam, ndege yake ilitunguliwa vitani na akakaa miaka mitano kama mateka wa wakati wa vita ambapo  aliteswa sana jambo lililomfanya kulemaa, ulemavu ambao aliishi nao maisha yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles