27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

WAPINZANI KENYA WATISHIA KUSUSIA UCHAGUZI

NAIROBI, KENYA


MUUNGANO wa upinzani nchini Kenya NASA, umetishia kuandamana na kususia Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8 iwapo Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) haitafutilia mbali rufaa iliyowasilisha kuhusu namna ya utangazaji wa matokeo rasmi ya urais.

IEBC ilikata rufaa katika Mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kuruhusu matokeo ya kura za urais kutangazwa katika kituo chao cha kukusanya matokeo.

Huku zikiwa zimesalia siku 84 uchaguzi mkuu ufanyike, umekuwa mchezo wa paka na panya kati ya chama kinachotawala cha Jubilee na NASA huku lawama zikitoka kila upande kushutumiana.

Upinzani unadai Jubilee inaitumia IEBC kubatilisha uamuzi wa mahakama uliotolewa mwezi uliopita, ambao uliwaruhusu kuwa na kituo chao cha kuhesabu kura.

Kiongozi wa walio wengi bungeni Adan Duale alidai  upinzani una njama ya kuiba kura kutumia mfumo wa kielektroniki.

"Tunajua wanaweka kituo cha kukusanya matokeo nchini Tanzania na watakapoweka kituo hicho watavuruga mtandao wa IEBC na wanataka kutumia matokeo ya kugushi kujitangaza washindi,” alisema.

Upinzani unataka kura za urais zihesabiwe na kutangazwa katika vituo vya maeneo ya uwakilishi bungeni jambo ambalo IEBC imepinga.

Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati alifafanua uamuzi wao, akisema, "Vyama vya kisiasa na vyombo vya habari vina uhuru wa kukusanya matokeo ya chaguzi kwa matumizi yao lakini ni wajibu wa tume ya IEBC kutangaza matokeo hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles