24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

TRUMP ADAIWA KUFICHUA SIRI ZA KIJASUSI KWA URUSI

WASHINGTON, MAREKANI


RAIS wa Marekani, Donald Trump anadaiwa kufichua taarifa nyeti za kijasusi kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov kuhusu operesheni iliyokuwa inapangwa dhidi ya wanamgambo wajiitao Dola la Kiislamu (IS).

Katika sakata jingine linaloukumba utawala wa Rais Trump ambaye hajakaa madarakani kwa muda mrefu, Gazeti la Washington Post ndilo lililoripoti suala hilo, ambalo Ikulu ya Marekani imeitaja kuwa ya uongo.

Tangu kuingia madarakani Januari mwaka huu, Trump amejikuta akijitosa kutoka sakata moja hadi jingine.

Katika taarifa zilizochapishwa juzi, Washington Post imenukuu duru kutoka kwa maofisa wa zamani na wa sasa wa Marekani ambao walisema Rais Trump alitoa taarifa nyeti za kijasusi kwa Lavrov na Balozi wa Urusi nchini Marekani Sergey Kislyak wakati walipokutana kwa mkutano wiki iliyopita Ikulu mjini hapa.

Taarifa hizo zilitoka kutoka kwa mmoja wa washirika muhimu wa Marekani anayehusika katika vita dhidi ya IS, ambaye hakuipa Marekani ruhusa ya kuzitoa taarifa hizo zinazohusiana na mipango ya kigaidi ya IS kwa Urusi.

Licha ya kuwa Rais ana mamlaka ya kufichua hata taarifa nyeti za kijasusi lakini katika kisa hiki hakushauriana na mshirika aliyezitoa taarifa hizo.

Kwa mujibu wa maafisa wa kijasusi, ambao hawakutaka kutambulika, kutolewa kwa taarifa hizo kunahujumu ushirikiano wa kubadilishana taarifa za kijasusi kati ya Marekani na washirika wake.

Mshauri wa masuala ya kitaifa ya usalama wa utawala wa Trump H.R McMaster aliwaambia waandishi wa habari kuwa taarifa hizo za kuvujishwa kwa taarifa nyeti za kijasusi si za kweli akiongeza kuwa Trump na viongozi hao wa Urusi walitathmini vitisho mbali mbali vya kiusalama ikiwemo kitisho kinacholenga safari za anga.

Licha ya maafisa wa ngazi ya juu wa utawala wa Trump kukanusha taarifa hizo, wabunge wa chama cha Democratic wameitaja mienendo ya Trump kuwa hatari na isiyojali.

Mbunge wa Chama cha Republican Bob Corker anayesimamia kamati ya Seneti ya masuala ya kigeni ameyataja madai hayo ya kutia wasiwasi mkubwa iwapo yatabainika kuwa ya kweli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles