27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

WAPINZANI KENYA WAAHIDI KUSHIRIKIANA

NAIROBI, KENYA


Raila Odinga, Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi na Moses WetangulaVIONGOZI wa vyama vya upinzani wamekutana mjini hapa juzi wakiapa kushirikiana ili kuing’oa madarakani Serikali ya Jubilee kupitia muungano wao mpya wa National Super Alliance (Nasa).

Viongozi hao, Raila Odinga, Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi na Moses Wetangula walitoa ahadi hiyo walipokutana kwenye Ukumbi wa Bomas.

Ajenda kuu ya mkutano huo ilikuwa kudhihirisha umoja miongoni mwa vigogo hao, ambao tayari wametangaza nia ya kuwania urais wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti,8 mwaka huu.

Zaidi ya wajumbe 4,000 wa vyama vya ODM, Wiper, Ford Kenya, Amani National Congress (ANC), na kile cha KANU walihudhuria mkutano huo.

Lengo kuu likiwa kutiwa saini makubaliano ya kubakia pamoja kwa viongozi wa vyama, kushirikiana kampeni na kubainisha ni nani hasa watakayemuunga mkono kupeperusha bendera kuwania kiti cha urais wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

Vigogo hao wamesisitiza umuhimu wa kuhakikisha makubaliano hayo yanatekelezwa.

Akiishtumu Serikali ya Jubilee, kinara wa muungano wa CORD, Raila Odinga, alisema licha ya kutoyakubali mageuzi yaliyofanywa sheria za uchaguzi hawatashiriki maandamano katika kipindi cha siku 30 zijazo.

Aidha amesema watahakikisha uchaguzi mkuu ujao unaandaliwa kwa njia huru na ya haki ili kufanikisha ajenda yao ya kuiondoa Jubilee mamlakani.

Kwa upande wake Kalonzo amebadili msimamo wa awali wa kutokubali kuachia nafasi ya kuwania urais, akisema yu tayari kumuunga mkono atakayeteuliwa kupeperusha bendera ya NASA, lengo likiwa kuondoa Jubilee mamlakani.

Wamewashutumu viongozi wa Jubilee kutokana na kukithiri kwa ufisadi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles