26 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

WAOMBWA KUTENGA MAENEO YA UWEKEZAJI

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


BALOZI wa Tanzania  Kenya, Dk. Pindi Chana ameziomba serikali za mitaa kutenga maeneo ya ardhi kwa ajili ya  kujenga kanda maalum za uwekezaji  kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa nchini na kuepelekwa nje ya nchi.

Dk. Chana alitoa kauli hiyo jana alipotembelea Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji  (EPZA)   Mabibo External kama sehemu ya ziara iliyofanywa na mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbal   kujionea shughuli zinazofanywa na mamlaka hiyo.

“Ni muhimu kwa halmashauri za serikali za mitaa zikatenga maeneo hayo  wawekezaji wapate kwa urahisi ardhi ya kujenga viwanda,” alisema.

Dk. Chana aliongozana na Balozi Omary Yusuf Mzee (Algeria), Balozi Fatma Rajab (Qatar), Balozi Grace Mgovano (Uganda)  na Balozi Matilda Masuka (Korea Kusini).

  Balozi Mzee alishauri itolewe elimu kwa wanasiasa na wananchi wa kawaida juu ya umuhimu wa kutoka misamaha ya kodi kwa wawekezaji katika sekta ya viwanda.

“Umekuwapo upotoshaji juu ya misamaha inayotolewa wakati ina mchango mkubwa katika kuvutia wawekezaji ambao hutoa ajira kwa Watanzania na kuchangia katika pato la uchumi wa nchi,” alisema.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia, alisema Tanzania ina rasilimali zote muhimu katika kuchochea uchumi wa viwanda.

Alisema utafiti uliofanywa na EPZA katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Shinyanga umeonyesha kuwapo  a faida kubwa inayotakana na wawekezaji walionufaika na misamaha ya kodi katika kanda maalumu za uwekezaji.

Akizungumza baada ya ziara hiyo, Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Fatma Rajab, aliahidi kutafuta fursa za mafunzo wa Kitanzania  kukidhi mahitaji ya uwekezaji katika viwanda ambao unapigiwa chapuo na serikali ya awamu ya tano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles