27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MITAMBO MIPYA DAWASA KUFANYIWA MAJARIBIO KESHO

Na MWANDISHI WETU-  BAGAMOYO


MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kesho inatarajia kuwasha mitambo yake ya maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini baada ya kufanyiwa upanuzi mkubwa.

Mitambo hiyo miwili imefanyiwa upanuzi kwa teknolojia ya kisasa  kuongeza uwezo wa kuzalisha maji ya kutosha kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ambayo ilikuwa na matatizo makubwa ya kukosekana na maji kwa miaka mingi.

Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Syprian Luhemeja alikuwa akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) juiz.

Alisema mitambo hiyo miwili itakuwa kwenye majaribio kwa mwezi mzima na aliwahakikishia  wakazi wa Dar es Salaam na Pwani kwamba hata yale ‘mabomba ya Mchina’ yataanza kutoa maji kama kawaida.

  Luhemeja alisema Mradi wa Ruvu Juu una thamani ya Dola za Marekani milioni 39.7 zilizotolewa na Serikali ya India kwa mkopo wa masharti nafuu.

“Mkandarasi amekamilisha uzalishaji  wa majaribio,  kilichobaki ni pamoja na kuvuta umeme mkubwa kutoka Chalinze, kazi ambayo itakamilika kabla ya Machi 31 mwaka huu.

“Kukamilika kwa mradi wa Ruvu Chini kutapunguza kero ya maji kwa wakazi wote wanaotumia maji kutoka mfumo wa Ruvu Chini ikiwamo Bagamoyo na maeneo mengi ya   Dar es Salaam.

  Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA, Profesa Felix Mtalo aliiomba PAC kusaidia kuweka msukumo kwa taasisi za Serikali kulipia bili za maji   miradi hiyo mikubwa iweze kuwa endelevu kwa manufaa ya taifa.

“Mitambo kama hii imetumia fedha nyingi, gharama za kutibu maji pia ni kubwa mtusaidie kuweka msukumo kuhakikisha kila anayetumia huduma hii analipia,” alisema Profesa Mtalo.

  Kaimu Mwenyekiti wa PAC, Dk Hadji Mponda aliwataka DAWASA kukarabati miundombinu ya mabomba ili kudhibiti upotevu mkubwa wa maji ambao unasababisha maeneo mengine kukosa maji. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles