26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

WANNE WAFARIKI KWA MATUKIO TOFAUTI TANGA

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Tanga, Benedict Wakuyamba
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Tanga, Benedict Wakuyamba

Na AMINA OMARI – TANGA

WATU wanne wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa katika matukio mbalimbali yakiwamo  mauaji ya kugombea mpaka wa eneo la makazi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Tanga, Benedict Wakuyamba, alisema tukio la kwanza ni la mauaji lililotokea Desemba 10, mwaka huu, katika Mtaa wa Msakangoto jijini Tanga.

Katika tukio hilo, Kamanda Wakuyamba alisema watu wawili walipoteza maisha na mmoja alijeruhiwa katika ugomvi wa kugombea mpaka wa shamba.

“Vifo hivyo vilitokea baada ya Venance Fabian kuuawa kwa kuchomwa kisu na jirani yake, Salum Ramadhani, ambaye naye alijiua kwa kutumia kisu hicho hicho.

“Salum kabla ya kujiua, alimshambulia kwa kisu mke wa Venance na kumsababishia majeraha mwilini na baada ya tukio hilo, ndipo naye alijichoma kwa kisu na kufa kwenye eneo la tukio.

“Tukio jingine ni la ajali iliyohusisha gari aina ya Prado, lenye namba za usajili T 299 AVX, iliyotokea wilayani Korogwe kutokana na mwendokasi.

“Katika ajali hiyo, watu wawili walifariki dunia papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa,” alisema Kamanda Wakuyamba.

Aliwataja waliofariki kwenye ajali hiyo kuwa ni Sanula Said na Waziri Mbwambo na majeruhi ni dereva wa gari hilo, Mohamed Mkawachi, Saada Said, Salha Said na Issa Ramadhan.

Katika ajali nyingine, gari la mizigo lenye namba za usajili T 260 DBW, liliacha njia na kupinduka  na kujeruhi watu wawili ambao ni dereva, Salum Athuman na Yussuph Seleman.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles