27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WANAWAKE WAJUMUISHWE KATIKA  UCHIMBAJI MADINI

 

Na Amina Omari,aliyekuwa MOROGORO



TANZANIA ni miongoni mwa  nchi yenye hazina ya madini mbalimbali yakiwemo  madini adimu kama ya vito na metali ambapo mchango wa sekta ya madini ni muhimu  katika ukuaji wa uchumi.

Sekta hiyo ni moja wapo ya fursa zinazosaidia kutengeneza  ajira zilizorasmi na zisizo rasmi na kwa kuwawezesha wananchi kupata kipato cha uhakika  na
pamoja na serikali kwa ujumla.

Hata hivyo mikakati ya serikali ni kuhakikisha kwamba rasilimali hiyoya madini inalinufaisha Taifa na watu wake kwa kuweka mipango madhubuti  na endelevu ambayo itawezesha kufikia lengo hilo.
Moja ya hatua ambayo serikali ya awamu ya tano imeweza kuchukua  ili  kudhibiti ulanguzi wake ni pamoja na kutoruhusu malighafi za madini hayo kusafirishwa nje ya nchi  bila kuongezwa thamani.

hatua hizo ikiwemo  kuweka na kusimamia mfumo thabiti wa kukagua shughuli za  migodi, kukusanya takwimu za madini na kufuatilia maduhuli yake yatokanayo , na madini kwa malengo mapana ya kuongeza mapato ya Serikali.

Wakati serikali ikiweka mazingira wezeshi kwa wachimbaji wa madini kuweza kunufaika na raslimali hiyo nao wadau mbalimbali wameanza   kuunga mkono juhudi hizo za serikali.
Ambapo  kwa hivi karibuni taasisi ya Best Dialogs ya nchini Marekani waliweza kuendesha utafiti kuhusu changamoto zilizoko kwenye sekta ya madini nchini ili kusaidia juhudi za serikali katika kufufua uchumi wa
sekta hiyo.

Hata hivyo utafiti huo  ulilenga katika kuibua changamoto zilizoko  katika  sekta hiyo hususani kwa upande wa wanawake ambao katika shughuli za umiliki wa migodini na uchimbaji  ni wachache .
Ambapo baadhi ya changamoto zilizoweza kubainika ni kutoeleweka kwa  sera ya madini kwa wachimbaji wenyewe na baadhi ya watendaji wa  serikali,  mitaji midogo , ushiriki mdogo wa wanawake katika shughuli za
uchimbaji na umiliki wa migodi.

Yunus Negele ni Mwenyekiti wa chama cha Wachimbaji wanawake nchini TAWOMA ambapo anasema kuwa kupitia utafiti huo waliweza kubaini kuwa ukosefu wa mitaji  umesababisha wanawake wengi kutoweza kushiriki  katika shughuli za uchimbaji na umiliki.

Anasema kuwa kutokana na ugumu wa sekta hiyo umesababisha wanawake  kutoweza kushiriki katika shughuli hiyo ya kiuchumi hivyo kukosa  nafasi ya kuweza kujiongezea kipato chao.

“Unajua shughuli za uchimbaji zinahitaji mitaji hivyo kupitia utafiti  huo tumeweza kupata mwanga kuwa kumbe nasi tunanafasi ya kushiriki ipo  kama tutaweza kujiunga  katika vikundi na kupata mitaji ambayo
itasaidia kuendesha shughuli hizo,”amesema Negele.

Pia Amesema kuwa utafiti huo umeweza kubaini kuwa uchimbaji wa  kuhamahama nao ni  moja ya changamoto kubwa inayowakabili wachimbaji  wengi kwa sasa hivyo kujikosesha fursa ya mapato.
Anasema kuwa kwa wachimbaji wadogo wamekuwa wanaendesha shughuli za uchimbaji kiholela kutokana  na kutokuwa na vifaa vya kubaini eneo lenye  madini hivyo kuishia kuendelea na uchimbaji wa kuhamahama kutoka eneo  moja kwenda jingine.

Aidha Negele amesema kuwa kwa kiasi kikubwa  wachimbaji wadogo wengi  hawana elimu ya kutosha kuhusu madini wala maeneo ambayo yanamadini hivyo kuishia kuendesha shughuli za uchimbaji kwa kubahatisha na  kwa mazoweya.

“Kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu madini pamoja na maeneo yenye  madini ni changamoto inayowakabili wachimbaji hususani wadogo  huku  wakitumia zana duni ambazo huishia kupata mavuno machache,”amesema
Mwenyekiti huyo.

Jambo hilo linaungwa mkono na Lucas Chuwa ambaye anasema kuwa  wachimbaji wadogo wadogo wamekuwa wakichimba madini ambayo kwa  asilimia kubwa hata hawajui thamani yake.
Anasema kuwa hawana uelewa wa aina ipi ya madini inayohitajika sana  katika soko hivyo wakati mwingine huishia kupata hasara huku wakiwa wametumia nguvu kubwa katika uchimbaji.

“Unakuta kama madini ya vito ambayo si rahisi kupatikana  lakini hujui kito aina ipi ndio inahitajika sana sokoni  hivyo unaishia kuchimba mali ambayo  sio yenyewe  na ukiipeleka sokoni  uuzaji wake aidha unakuwa mgumu au unauza kwa  bei ya hasara,” amebainisha Chuwa
Aidha ameongeza kuwa wachimbaji wengi wadogo hawana ufahamu wa kutosha kuhusu aina ya madini wanayoyachimba hivyo  kutofikia  malengo yao.

 

“Serikali ingeangalia uwezekano wa kuwafanya wamiliki wa ubia na wawekezaji wachimbaji ambao wanagundua maeneo ya madini kabla ya  kupima maeneo na kuwamilikisha wawekezaji ,”amesema Chuwa.
Anasema kuwa hatua hiyo itawezesha wachimbaji wadogo kukua kishughuli na  kiutendaji badala ya kuchimba kwa kutumia zana duni sasa wataweza
kutumia zana bora na za kisasa.

Hata hivyo Mchimbaji Said Bomani amesema kuwa kutokueleweka kwa sera za madini kwani imeandikwa kwa lugha ya kingereza  hivyo kusababisha wadau wengi kutoweza kuelewa kilichomo ndani ya sera hiyo.

“Ingependeza sera hiyo iweze kufikia hadi katika ngazi za mikoa na  wilaya ili watendaji wa serikali waweze kuielewa kwani wamekuwa  wanatoa maagizo ambayo wakati mwingine yanapingana na sera hiyo,”amesema Bomani.
Aidha ameishauri serikali kuona namna bora ya kuyagawa maeneo yenye madini ambayo wawekezaji wameshindwa kuyafanyia kazi na kuyagawa kwa wachimbaji wadogo ili waweze kuyaendeleza.

Nae Negele ameipongeza Serikali kwa kuendesha zoezi la urasimishaji wa leseni za uchimbaji wa madini ili kuweza kutambua idadi kamili ya wachimbaji nchini kwa ajili ya malengo ya uchumi endelevu.
Amesema kuwa kukamilika kwa zoezi hilo kutasaidia kujua idadi kamili ya leseni,na serikali itaweza kujua makusanyo halisi ya mapato yatokana na na leseni za uchimbaji huku kwa  upande wa uchimbaji  kutaweza kuibua fursa ya ajira rasmi.

Kwani zoezi hilo litaweza kusaidia kuepuka uchimbaji wa kuhamahama  unaoendelea kufanywa na wachimbaji hususani wadogo kwa ajili ya  kutafuta madini .
Huku akiiomba serikali kuwasaidia wachimbaji wadogo fedha za mikopo kwa ajili ya kukuza shughuli zao ili waweze kufanya uchimbaji vizuri kwa kutumia vifaa vya kisasa.

“Mchakato wa uanzishwaji wa viwanda vya kuchakata madini utasaidia  kuvutia wachimbaji wengi hivyo ni wakati mwafaka  kwa serikali kuweka mazingira bora ya sekta hiyo iweze kunufaisha wananchi wake kiuchumi,”amesisitiza  Mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake Katibu wa TAWOMA Salma Kundi amesema kuwa ukosefu wa  taarifa sahihi za kijiolojia umesababisha wachimbaji wengi wadogo  kukata tamaa ya kuendelea na shughuli za uchimbaji.
Anasema kuwa ukiangalia idadi ya leseni za uchimbaji imeweza kushuka  kwani mwaka 2016 kulikuwa na maombi 9827 ukilinganisha na mwaka 2017
maombi 5171 pekee.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles