23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

FANGASI ZA MAHINDI, KARANGA ZINAONGEZA KANSA ISIYOTIBIKA

 

Na Gordon Kalulunga, Mbeya


NGONO zembe yahimiza saratani ya kizazi wakati Saratani ya matiti yaliza wanawake wengi na hivyo kuufanya ugonjwa wa kansa kuwa wa kujogopewa kwani unapatikana kwa kufanya ale ya kawida kabisa katika maisha.
Chakula chetu na namna tunavyojamiana ni suala muhimu kuzingatia kwani ni vyanzo vikubwa vya saratani kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalamu wa afya nchini na nje ya nchi..

Sumu kuvu iitwayo (Aflatoxin) inayotokana na fangasi waitwao aspergillus wanaoshambulia mimea na kupatikana zaidi katika punje za Mahindi na Karanga, inasababisha ugonjwa wa kansa ya ini ambayo haina
tiba.
Uchunguzi uliofanywa na Mwandishi wa habari hii, umebaini kuwepo kwa hatari kubwa ya ongezeko la kansa hiyo kwa watumiaji wa bidhaa hizo wakiwemo wanywaji wa Pombe za kienyeji zitokanazo na Mahindi “kuvundikwa’’ kusudi iwe ‘mkangafu’ haifai kuinywa.

Njia inayotajwa kuwa inaweza kuzuia hatari hiyo ili vyakula visishambuliwe na fangasi hawa ni kutunza mahindi/karanga katika sehemu ambazo hazina unyevu, kutovuna mazao kabla ya wakati na kuzuia mazao
kushambuliwa na panya au wadudu wengine, jambo ambalo wakulima wengi na wafanyabiashara hawafanyi hivyo.

Zaidi wakulima na wafanyabiashara wengi wakivuna Mahindi huwa wanayahifadhi kwa kutumia sumu za maji zisozoruhusiwa kuhifadhia nafaka hizo hali ambayo inaongeza hatari ya punje za mahindi kuwa na
ukungu kwenye kiini.

Watu wanaoishi katika nchi masikini ikiwemo Tanzania, wako katika hatari kubwa zaidi ya kupata kansa ya aina hii kwasababu watu wengi wanaoishi katika maeneo haya hutumia sana mahindi kama chakula chao cha kila siku.
Jinsi gani mtu ataathirika itategemea na hali ya afya ya mgonjwa, kiwango cha sumu alichokula na muda ambao amekua akitumia hivyo vyakula na nguvu za kinga alizonazo mgonjwa kwani ikisha ingia mwilini nadra kutoka au kufa fangasi hizi.

Mwaka jana 2016 Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzanisa (TFDA) walitoa matokeo ya tafiti zao na kukuta viwango vikubwa vya sumu hii kwenye mahindi na unga uaouzwa.

Daktari bingwa wa magonjwa ya kansa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya  Dr. Kelvin Kanama anathibitisha kuwa sumu hiyo inayopatikana kwenye mahindi na karanga inasababisha kansa ya ini.
Anasema kuwa kwa sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa kansa katika hospitali hiyo ingawa takwimu sahihi hutolewa na Hospitali maalum ya matibabu ya ugonjwa huo  ya Ocean road Jijini Dar Es Salaam.

“Ila kansa za kawaida taarifa  zake tunazo. Kwa wagonjwa wanaolazwa katika wodi za idara ya tiba za wanawake na wanaume saratani inayoongoza ni ‘kaposi sarcoma’ ambayo inawapata sana waathirika wa virusi vya ukimwi,” anaeleza daktari huyo.

Alisema kansa hiyo inaongoza kwa wodi zote mbili za wanawake na wanaume.
“Kwa upande wa wanawake kiujumla saratani zinazoongoza ni ya ziwa  namba moja ikifuatiwa na ya shingo ya kizazi namba mbili. Yaani breast cancer na cervical cancer,” anasema daktari huyo.

Anatoa ushauri kuwa cha muhimu kwa upande wa saratani ya ziwa ni kwa mwanamke kugundua dalili mapema na kuweza kuwahi hospitali kabla haijasambaa na kuwa ngumu kuitibu, hii ni pamoja na kuangalia kamakuna uvimbe wowote kwenye mojawapo ya ziwa, maumivu na kubadilika kwa  ngozi.
Alipoulizwa kuhusu ongezeko la kansa hizo alisema kuwa idadi  inaongezeka kwasababu uwezo wa kuitambua umeongezeka zaidi tofauti na hapo awali ingawa wengi hawafiki hospitalini kwa ajili ya uchunguzi.

“Kwa upande wa saratani ya kizazi njia bora zaidi ya kuizuia ni kutokufanya ngono zembe,  sababu kirusi kinachosababisha saratani za  kizazi kinaweza ambukizwa kwa njia hii. Kirusi hiki kinaitwa Human papilloma virus (HPV)” anasema Dk. Kanama.
Kansa zote zinauwezekano mkubwa wa kutoa matokeo mazuri ya tiba kama  zitagundulika mapema, na hiyo ndio changamoto kwani inaingia kimya kimya na taratibu.

Mwisho.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles