25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

WANAWAKE WAHIMIZWA KUJITOSA SEKTA YA MADINI

NA BRIGHITER MASAKI (TSJ) – Dar es Salaam


mehjabeen-alarakhiaCHOMBO cha Umoja wa Mataifa kinachosimamia usawa wa kijinsia na uwezeshaji kwa wanawake (UN Women), kimetoa majibu ya utafiti juu ya changamoto na fursa zilizopo kwa wachimbaji madini wanawake.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi mwezeshaji wa wanawake kiuchumi (UN Women), Mehjabeen Alarakhia, alisema utafiti huo umetoa majibu mengi kuhusu fursa na changamoto za uchimbaji wa madini kwa wanawake.

“Changamoto zilizopo katika uchimbaji wa madini wanatakiwa kutumia kama fusra katika sera ya utekelezaji wa uchimbaji madini kuimarisha sera, vifaa vya uchimbaji wa madini kwa wachimbaji wadogo wadogo ambao hawana uwezo wa kupata mashine za kuchimbia kuwawezesha mtaji wa kuendesha biashara,” alisema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wahandishi wa Habari Wanawake (Tamwa), Edda Sanga, alisema sekta ya madini ni kama kitu kipya kwa wanawake ambao hapo mwanzo walikuwa wakitoa msaada wa kuwapikia chakula wachimbaji migodini.

“Kuna mwanamke mmoja ambaye ni jasiri, jina lake hakutaka litajwe, ambaye aliingia mgodini kama mchimbaji lakini alijitambulisha kama mwanamume kwa sababu wanaume wana dhana potofu kusema kuwa mwanamke akiingia mgodini mgodi hautemi, ni nuksi,” alisema Sanga.

Kwa upande wake, ofisa mwandamizi  Ubalozi wa Canada, Stephen Kijazi, alisema matokeo ya utafiti uliofanywa na UN Women yamewafungua macho wadau wa sekta ya madini juu ya changamoto hizo kwa wanawake sambamba na vikundi pamoja na kuwajengea uwezo, kuwawezesha mitaji na kuwasaidia kufanya kazi zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles