31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA MWANAFUNZI

Na SAMWEL MWANGA – MASWA


jelaMAHAKAMA ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imemhukumu Gervas Elihuruma (20), mkazi wa Kijiji cha Sangamwalugesha wilayani humo kifungo cha miaka 30 na kuchapwa viboko 12 baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita.

Hukumu hiyo imetolewa juzi na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Maswa, Fredrick Lukuna, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka.

Hakimu Lukuna alisema kuwa ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia mbaya ya kutaka kutenda kosa kama hilo katika jamii.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi wa Polisi, Nassibu Swedy, kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Septemba 20 mwaka 2015 saa 7.00 mchana katika Kijiji cha Sangamwalugesha wilayani Maswa.

Swedy aliieleza mahakama kuwa mshtakiwa alimrubuni na kisha alimbaka mwanafunzi huyo wa kike mwenye umri wa miaka 15 aliyekuwa darasa la sita katika Shule ya Msingi Sangamwalugesha.

“Mshtakiwa baada ya kumbaka, alimtorosha mwanafunzi huyo na kwenda naye mjini Kateshi mkoani Manyara na kuishi naye kama mke takribani mwezi mmoja,” alisema Swedy.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles