27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wanawake wachora nyuso zao kwa damu ya hedhi

Na Mwandishi Wetu

AKIWA na umri wa miaka 27, Lauraa Teixeira, mkazi wa Amerika Kaska­zini, kila anapoingia kwenye hedhi, hukusanya damu yake na kupaka usoni, huku ile inayobaki akiichang­anya na maji kwa ajili ya kumwagilia mimea.

Utaratibu huu unaitwa ‘kupanda mbegu ya mwezi’ ambapo ni utamaduni ulioanzish­wa na mababu waliokuwa wakisherehekea damu ya mwezi na kuitambua kama ishara ya uzazi.

Wanawake wanaofuata utamaduni huu wana namna yao ya kusherehekea ‘miezi’ yao, ambayo waliona kama ilikuwa na awamu, ambapo kila mzunguko ulikuwa na maana yake.

Akizungumza na BBC, Laura anasema alikuwa na maneno maalumu ya kumwagilia mimea, akiiambia: “Samahani, nisamehe, ninakupenda na ninakushukuru.” Huwa anarudia maneno haya.

Anasema: “Mimea huota na kuwa mizuri na kupokea virutubisho vingi.”

Damu ya hedhi husaidia kurubisha mimea

Anasema kila anapofuta damu hiyo ya mwezi mwilini mwake, hufumba macho yake na kujihisi mwenye shukrani na nguvu tena.

Kwa Laura, mila hii ni huwaongezea nguvu wanawake.

“Moja ya ubaguzi mkubwa kabisa ni mtazamo hasi wa jamii kuhusu damu ya mwezi na jinsi ambavyo wanawake bado wanahisi aibu kuhusu hedhi yao,” anasema.

Naye Mwanasaikolojia, Mcheza dansi na mwandishi dansa, aliyeanzisha kampuni inayotekeleza mila hiyo – World Seed Your Moon Day, mwaka 2018, Morena Cardoso , anasema kupanda mwezi ni kitu rahisi mno, lakini chenye nguvu kubwa, kinachoponya na zoezi la kina kwa mwanamke.

Morena akiwa amejichora kwa damu ya hedhi

Mwaka jana, takribani watu 2,000 wali­panda mbegu za damu yao ya hedhi kwa pamoja katika maeneo ya umma.

Morena anasema wazo la tukio hilo, ni kwamba damu ya hedhi si sababu ya kum­fanya mwanamke aone aibu, bali anapaswa kujivunia na humpa nguvu.

‘Kazi ya kiroho ya wanawake’

Kwa mujibu wa Morena, miongoni mwa tamaduni za wazawa Amerika Kaskazini ikiwamo Mexico na Peru, damu ya hedhi ili­kuwa ikimwagwa ardhini kuifanya iwe yenye rutuba na yenye kumea mimea kwa wingi.

Iliwakilisha muda wa ushirika na kazi ya kiroho ya wanawake, pia ibada ya wanawake wanaojiandaa kuwa na heshima ya kike.

Daniela Tonelli Manica, ambaye ni Mtaalam wa Historia ya Binadamu katika Chuo Kikuu cha Brazil Unicamp, aliyefanyia utafiti suala la hedhi miongoni mwa jamii kwa miaka 20, anasema katika jamii nyingine kuna mitazamo hasi kuhusu damu ya hedhi.

Anasema: “Damu ya hedhi huangaliwa kama utokwaji wa damu usio na maana, am­bao huwekwa katika kundi moja na kinyesi na mkojo – kitu ambacho unamalizana nacho msalani, hakipaswi kuonekana machoni pa watu.”

Katika miaka ya 1960s, vuguvugu la haki za wanawake lilitaka kubadilisha mitazamo hii, likiwataka wanawake kuzungumzia zaidi juu ya miili yao na kuheshimu maumbile yao.

Wasanii walikuja baadae kuvumbua ishara ya damu ya hedhi kuelezea maoni yao ya kisiasa kuhusu masuala ya mazingira, ngono na jinsia.

Yatumika kumwagilia maua

“Nilidhani ilikuwa ni haki na jambo sahihi kurejesha kwa dunia kile inachotupa­tia,” anasema Renata, mwanamke ambaye hukusanya damu yake ya hedhi bafuni na kuimwagilia kwenye mimea ya maua ya aliyoipanda kando ya nyumba yake kwenye vyungu.

Renata pia hupanda mimea ya minti ambayo haimwagilii na damu yake ya hedhi na inaonekana kuwa ‘dhaifu’ utadhani ina ‘utapiamlo.’

Mara ya kwanza Renata mwenye umri wa miaka 43, alipopata hedhi, akiwa na miaka kumi na zaidi, alikuwa ameambiwa kuwa: “Sasa wewe ni mwanamke mchanga, utaanza kuvuja damu kila mwezi na watu hawapaswi kufahamu hilo.”

Awali aliiona hedhi yake kama maudhi ya mara kwa mara na aliwaonea wivu wanaume ambao hawapati hedhi. Lakini sasa anaiona kama kitu ‘kitakatifu.’

Maua yakimwagiliwa kwa damu ya hedhi

Utafiti

Utafiti wa dunia waliofanyiwa wanawake 1,500 walio na umri kati ya miaka 14 hadi 24 unaonyesha ni kwa kiwango gani suala la hedhi bado ni mwiko katika jamii nyingi.

Kwa mujibu wa utafiti – ulioagizwa na Johnson & Johnson na kufanyika katika nchi za Brazil, India, Afrika Kusini, Argen­tina na Ufilipino – wanawake wanahisi aibu wanapoazima sodo (vitambaa vya hedhi), wanaoonekana wakizihifadhi baada ya kuzi­tumia na hata kusimama kutoka kwenye viti vyao wanapokuwa katika kipindi cha hedhi.

Utata

Lakini si kila mmoja yuko tayari kukubali mila ya kupanda mbegu ya mwezi na hivyo ndivyo Laura alivyoibua mjadala mwezi uliopita baada ya kutuma picha ya ‘selfie’ iliyoonyesha uso wake na kifua vikiwa vime­pakwa damu ya hedhi.

“Nilikuwa na wafuasi 300 na nilifikiria utakuwa tu kama ujumbe wa kawaida niliou­tuma kwenye ukurasa wangu wa mtandao wa kijamii ili kumsaidia mwanamke mwing­ine kuelewa mada,” anasema.

Siku nne baadae, alibaini kuwa alikuwa amedhalilishwa kwenye mtandao wa In­stragram ambapo vibonzo vya akaunti ya Instagram vilitumwa kumkejeli.

Mchekeshaji mwenye utata nchini Brazil, Danilo Gentili, alifikiri kuwa lilikuwa jambo la maana kutuma picha kwa wafuasi wake wa Instagram milioni 17, akisema: “damu ya hedhi ni ya kawaida, kitu ambacho hakikuwa cha kawaida ni kuipaka kwenye uso wako.”

Lakini utani wake haukuwafurahisha wengi, majibu 2,300 yakiwa ni ya wale wal­ioonyesha kutofurahishwa nao.

Laura anasema kuwa yaliyotokea kuhusu ujumbe wake wa picha yanathibitisha tu jinsi suala la hedhi lilivyo mwiko.

“Watu wanafikiri kwamba ikiwa kama kitu si cha kawaida kwao, basi lazima kisikuba­like. Wanafikiri wanaweza kujificha nyuma ya simu zao za mkononi na kutumia maneno ya chuki kumuumiza mtu fulani,” anasema na kuongeza.

Mwaka jana watu 2, 000 walipanda mbegu za damu ya hedhi kwa pamoja katika maeneo ya umma
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles