RIYADH, SAUDI ARABIA
MAMLAKA za Saudi Arabia zimetoa leseni 10 za kwanza za kuendesha magari kwa wanawake juzi.
Tangazo hilo linakuja wiki moja tu kabla ya marufuku ya wanawake kuendesha magari kuondolewa kufuatia uamuzi wa mfalme Salman mwaka jana kuruhusu wanawake kuendesha magari.
Saudi Arabia ni nchi pekee duniani ambako wanawake hawaruhusiwi kuendesha magari, lakini hali hiyo itabadilika Juni 24.
Kiasi ya leseni 2,000 zinatarajiwa kutolewa kwa wanawake wiki ijayo, kwa mujibu wa taarifa kutoka wizara ya habari.
Wanawake ambao tayari wanamiliki leseni kutoka nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na Uingereza, Lebanon na Canada, walifanya majaribio mafupi ya kuendesha kabla ya kupewa haki hiyo nchini Saudi Arabia.