30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

MSHIRIKA WA RAIS TRUMP AKAANGWA MAHAKAMANI

WASHINGTON, MAREKANI


MSHAURI maalumu wa Marekani, Robert Mueller amedai aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampeni ya Rais Donald Trump, Paul Manafort alijaribu kuwarubuni mashahidi wa kashfa ya kushirikiana na Urusi kuingilia uchaguzi wa urais 2016.

Mueller, ambaye anaongoza uchunguzi kuhusiana na uwezekano wa ushirika baina ya kampeni ya Rais Trump mwaka 2016 na Urusi, alitoa madai hayo mahakamani juzi.

Katika shutuma hizo, Mueller anadai Manafort pamoja na mshirika wake, ambaye hakutajwa walijaribu kuwapigia simu na kutuma ujumbe wenye maandishi ya siri mashahidi wawili muhimu, Februari mwaka huu.

Wawili hao ni wanachama wa kundi la Hapsburg, chama kinachofanya ushawishi cha maafisa wa zamani wa Ulaya ambao walihamasisha maslahi ya Serikali ya zamani ya Ukraine.

Jaribio la Manafort kushawishi ushahidi wa mashahidi hao, ambao hawakutajwa katika waraka uliopelekwa mahakamani lilitokea wakati akiwa katika kizuizi cha nyumbani.

Kutokana na hilo, Mueller amemuomba jaji anayeshughulikia kesi hiyo kuitisha kikao juu ya kufuta uamuzi ambao uliruhusu Manafort kuachiwa huru kutoka kizuizi cha nyumbani hadi pale kesi yake itakapoanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles