23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

WANAUME WANAOTOA TALAKA ZA ‘PAPO HAPO’ KUFUNGWA JELA

NEW DELHI, INDIA


WANAUME waliopo katika ndoa ambao hujaribu kutoa ‘talaka tatu za papo hapo’ huenda wakahukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela chini ya rasimu ya sheria zinazopendekezwa nchini India.

Utamaduni huo unashirikisha mwanamume wa Kiislamu anayetamka talaka mara tatu kwa njia nyingi ikiwemo ujumbe mfupi wa maneno wa simu au barua pepe.

Agosti mwaka huu, Mahakama ya Juu ilitangaza kuwa aina hizo za talaka ni kinyume na Katiba, lakini maafisa wanasema zimekuwa zikiendelea tangu wakati huo.

Sheria hiyo pendekezi inatoa faini na usaidizi kwa wanawake walioathirika.

Muswada wenye sheria rasimu za kuwalinda wanawake sasa umetumwa kwa serikali za majimbo kwa majadiliano.

Sheria hizo zimewekwa ili kuhakikisha kuwa iwapo mume atamtaka mkewe kuondoka katika nyumba wanayoishi basi atoe ulinzi wa kisheria.

Chini ya sheria hiyo wale watakaopatikana na hatia hawataruhusiwa kuachiwa kwa dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles