23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

UHURU AWAPONGEZA POLISI KWA KAZI NZURI

NAIROBI, KENYA


PAMOJA na Jeshi la Polisi kushutumiwa na upinzani na wanaharakati wa haki za binadamu kwa kutumia nguvu kupita kiasi pamoja na mauaji ya wafuasi wa upinzani, Rais Uhuru Kenyatta amelipongeza kwa siri kwa kazi nzuri wakati wa uchaguzi mkuu.

Jeshi hilo linalaumiwa kusababisha vifo vya watu 50 wakati wa maandamano ya upinzani wakiwamo watoto wanne.

Mtoto wa hivi karibuni kuuawa alikuwa Geoffrey Mutinda (7), aliyeuawa na wanaodaiwa kuwa Polisi katika mtaa wa Pipeline, Nairobi mapema wiki iliyopita wakati maafisa hao walipokabiliana na wafuasi wa NASA.

Kwenye barua ya siri iliyotumwa kwenda makamanda wa vikosi vyote vya polisi nchini, Mkurugenzi wa Operesheni za Polisi, Benson Kibui alisema: “Nimeagizwa na Mheshimiwa Rais kutuma pongeza kwa maafisa wa vyeo vyote waliohusika katika uchaguzi wa 2017 kwa kazi nzuri mliyofanya.’

“Pia anawashukuru kwa kutekeleza majukumu yenu kwa mujibu wa sheria katika mazingira ya ushindani mkali kisiasa na hata wakati wa uchaguzi wa marudio ya urais. Tudumishe moyo huo wa kuhudumia taifa na wananchi wa Kenya,” ilisema barua hiyo ya siri ambayo baadhi ya vyombo vya habari vimeiona.

Rais alitoa ujumbe huu wa pongeza siku moja kabla ya familia za watu 26 waliouawa katika vurugu za kisiasa kuchukua miili ya wapendwa wao kuisafirisha sehemu mbalimbali kwa mazishi.

Miili hiyo ilikuwa imehifadhiwa katika vyumba vya kuhifadhi maiti vya Hospitali za City na Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Ripoti ya upasuaji ya miili hiyo iliyotolewa na mtaalamu wa afya wa serikali, Dk. Johansen Oduor ilionyesha kuwa watu 10 kati yao waliuawa kwa risasi.

Hata hivyo, polisi wamekanusha madai ya kuhusika na mauaji hayo wakisema waliouawa walikuwa majambazi walioshambuliwa na wafuasi wa NASA waliojitokeza kumlaki kinara wao Raila Odinga aliporejea kutoka Marekani wiki mbili zilizopita.

Tume ya Taifa ya Kutetea Haki za Binadamu (KNHRC), Halmashauri ya Kuchunguza Utendakazi wa Polisi (IPOA) ni miongoni mwa taasisi ambazo zimeilaumu polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya wafuasi wa NASA katika msimu wa uchaguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles