Aveline kitomary
Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu wa afya ya akili Tanzania, Isaack Lema amewashauri wanaume kulia ili kupunguza msongo wa mawazo ambao unaweza kupelekea kujiua.
Akizungumza katika mafunzo ya madaktari na wauguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alisema wanaume wanaongoza kujiua kuliko wanawake.
“Wanaume wanaongoza kujinyonga mara tatu kuliko wanawake hivyo ni bora wakalia ili kupunguza msongo wa mawazo,”alisema.
Hata hivyo Daktari bingwa wa afya ya akili Dk. Prexede Swai alisema wanaume wanaoongoza kujinyonga ni wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35.
“Asilimia kubwa ya watu wanaojiua ni vijana wengi wao ni kwasababu wanakutana na mazingira au jamii ambayo haiwasikilizi au kutafuta changamoto zao.