27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

‘Wanaume lieni kupunguza msongo wa mawazo’

Aveline kitomary

Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu wa afya ya akili Tanzania, Isaack Lema amewashauri wanaume kulia ili kupunguza msongo wa mawazo ambao unaweza kupelekea kujiua.

Akizungumza katika mafunzo ya madaktari na wauguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alisema wanaume wanaongoza kujiua kuliko wanawake.

“Wanaume wanaongoza kujinyonga mara tatu kuliko wanawake hivyo  ni bora wakalia ili kupunguza msongo wa mawazo,”alisema.

Hata hivyo Daktari bingwa wa afya ya akili  Dk. Prexede Swai alisema wanaume wanaoongoza kujinyonga ni wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35.

“Asilimia kubwa ya watu wanaojiua ni vijana wengi wao ni kwasababu wanakutana na mazingira au jamii ambayo haiwasikilizi au kutafuta changamoto zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles