25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

WANAOISHI NA UKIMWI WAPATA MILIONI 200/-

Na JUDITH NYANGE


ZAIDI ya Sh milioni 200 zimetolewa na Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA)   kuyasaidia mabaraza ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi   katika halmashauri nane za Kanda ya Mwanza.

Hatua hiyo ni  kuziwezesha kuchangia juhudi za serikali kufikia malengo ya taifa.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa NACOPHA, Deogratius Rutatwa alikuwa akizungumza juzi wakati wa kusaini mikataba ya utoaji wa ruzuku hiyo   Nyamagana, Ilemela, Musoma, Kahama, Sengerema, Nzega, Igunga na Muleba.

Alisema ruzuku hiyo imetolewa katika maeneo manane ya Kanda ya Mwanza kwa ajili ya kuwawezesha watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi kufikia lengo la taifa la 90 ya kwanza linalowataka watuwanaoishi na virusi vya Ukimwi kujua hali zao

Malengo hayo ya  taifa  ni kushawishi watu waweze kupima kujua afya zao,  waliopima na kugundulika kuwa na Virusi vya Ukimwi asilimia 90 waweze kuanza tiba   na wale walio kwenye tiba asilimia 90 kufikia mwaka 2020 virusi vyao viwe vimefubaa.

Alisema wanapaswa kuwa wamefanikiwa  kufikisha asilimia 92 ya watu waliofika katika vituo na kupima afya zao na kufahamu hali zao, wale waliokuwa watoro wa dawa wamewapata kwa asilimia 62 tangu kuanza kwa mradi huo.

“Si kila mtu ambaye hajapima anajua hali ya afya yake, mara nyingi watu kwa sababu hawajapima wanaweza kusema hawana maambukizi ya virusi vya Ukimwi ni vigumu kujua hali ya afya yako  kama hujapima.

Ili kufikia  malengo ya  taifa ni lazima watu waweze kujua afya zao, waliopima na kugundulika na virusi vya Ukimwi asilimia 90 waweze kuanza tiba    na wale walio kwenye tiba asilimia 90  kufikia 2020 virusi vyao viwe vimefubaa,” alisema Rutatwa.

Akizungumza kwa niaba ya Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mwanza, Victor Bundala, alisema mradi huo utakapoanza kutekelezwa utasaidia  katika juhudi za kupunguza maambukizi na kuwarudisha watoro wa dawa kwenye matibabu ndani ya  halmashauri mbalimbali  nchini.

Alisema sera ya taifa ya Ukimwi imeainisha misingi ya jamii na mtu mmoja mmoja  kuhakikisha wanazuia na kudhibiti Ukimwi kwa kutoa elimu na kuwa na mawasiliano na jamii, bila juhudi za baraza ugonjwa wa Ukimwi unaweza kuleta athari kubwa saana katika jamii na kwa uchumi wa nchi.

Rutatwa alitaka mradi huo kuwa chachu  ya mapambano dhidi ya Ukimwi katika halmashauri zao.

Alisema   endapo wataitumia ruzuku hizo vema mradi utasaidia kupunguza kasi ya maambukizi ya Ukimwi katika jamiii na kuongeza idadi ya watu waliopima na kutambua hali zao za maambukizi ya ukimwi kuanza tiba na kuendelea kubakia katika tiba hizo.

Mwenyekiti  wa eneo la Muleba,  Romad Thomas,  alisema walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya elimu duni  na  unyayapaa baridi.

Alisema    kupitia ruzuku watakayopatiwa wataongeza uhamasishaji, kuwafuatilia watoro wa dawa na vipimo  kwenye kata zinazotekeleza mradi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles