25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

WANANE WAMWAGIKIWA UJI WA CHUMA

unset

Na ABRAHAM GWANDU, ARUSHA

WAFANYAKAZI wanane wa kiwanda cha nondo cha Bansal Steel Rolling Mills Ltd, kilichopo eneo la Kisongo jijini Arusha, wamenusurika kufa baada ya kumwagikiwa na uji wa chuma uliokuwa ukichemka.

Tukio hilo lilitokea juzi asubuhi kiwandani hapo, wilayani Arumeru na majeruhi hao walikimbizwa katika Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center kwa matibabu.

Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo, daktari aliyewahudumia wagonjwa hao, Dk. Rose Kaaya, alisema aliwapokea majeruhi hao juzi asubuhi, wakiwa wameungua sehemu mbalimbali za miili yao.

“Tumepokea wagonjwa wanane walioungua sehemu mbalimbali na wengine wana majeruhi yaliyosababishwa na kujeruhiwa na vyuma wakati walipokuwa wakikimbia kujiokoa,” alisema Dk. Kaaya.

Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Hassan Guni (27), Christopher Semkiwa (24), Fred Sungi (21), Adrea Kihundwa (26), Calvin Langu (19), Saimon Mkumbo (34), Saimon Njuguna (25) na Tilak Tiwakraj (34).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles