29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Segerea wasafisha mfereji wa maji machafu

mfereji-wa-maji-machafuNa MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

WANANCHI wa Kata ya Segerea jijini Dar es Salaam, wameshiriki kufanya usafi wa mfereji wa Kumbwaya, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dk. John Magufuli la kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Operesheni hiyo imeanzishwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Bonnah Kaluwa (CCM), ili kuunga mkono jitihada za Rais Dk. Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi.

Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa kufanya usafi katika mitaa ya Machimbo na Segerea, Mwakilishi wa Mbunge huyo, Rutta Rucharaba, alisema kila wiki huwa wanachagua mitaa na kwenda kufanya usafi kwa kushirikiana na wananchi pamoja na viongozi wa mitaa husika.

Diwani wa Kata ya Segerea, Edwin Mwakatobe (Chadema), ambaye alikuwa miongoni mwa walioshiriki zoezi hilo la usafi alisema kwa ujumla zoezi hilo lilikwenda salama ingawa kulikuwa na majirani waliojaribu kuwazuia kufanya kazi hiyo.

Alisema walikwenda kufanya usafi kwenye mfereji huo kama sehemu ya kutekeleza wa agizo la Rais Dk. Magufuli, lakini alishangazwa na baadhi ya majirani waliojaribu kuwazuia ingawa hawakufanikiwa.

“Na tumeshangazwa kuona mtu amejenga ukuta kuzuia maji yasipite kwenye mfereji huu wa asili, hizi ni chuki binafsi maana haya maji yatapita wapi,” alisema

“Tumemwambia waziwazi yule aliyejenga ukuta kwamba  kuanzia leo aache kuibughudhi shule kwa kutoa taarifa za uongo serikalini kwa lengo la kueneza chuki baina ya wananchi na shule za Tusime, akijaribu kufanya hivyo atapambana na wananchi wa Kata ya Segerea na si Tusiime,” alisema.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Segerea, Karama Mkambaku, alisema mfereji huo ulioko kwenye bonde la Kumbwaya unapitisha maji mengi kutoka maeneo mbalimbali hivyo wameona ni busara kuusafisha mara kwa mara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles