Na Sheila Katikula, Mwanza
Wananchi wa Mkoa wa Mwanza na maeneo ya jirani wameobwa kujitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa CCM Kirumba uliopo wilayani Ilemala mkoani hapa machi 24, ili waweze kuuaga mwili wa hayati Rais Dk.John Mafuli aliyefariki Machi 17, mwaka huu.
Wito huo ulimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela wakati akizungumza na viongozi wa dini wa Kamati ya Amani ya Mkoa na Kamati ya Ulizi  jijini hapa alipokuwa akitoa ratiba ya kuaga mwili huo.
Alisema zoezi hilo litashirikisha wananchi kutoka sehemu mbalimbali ili waweze kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania hayati John Magufuli.
Ameongeza kuwa ni vema viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa liendelee kuwa na amani, utulivu na mshikamano uliopo nchini.
“Nawaomba viongozi wa dini muendelee kuliombea taifa na kutoa mahubili ya kuhamasisha amani na kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan aliyeshika nchi baada ya kutolea Kwa tukio hili,”alisema Mongela.
Naye Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani ya Mkoa ya viongozi wa dini Askofu wa Kanisa la Charismatic Episcopal Church of Tanzania C.E.C (T), Charles Sekelwa, amesema ni lazima kukubali ni  mapenzi ya mungu hayana makosa kwani kifo ni uwezo wa mungu na kila nafsi itaonja umauti Kwa upande wake  Sheikhe wa msikiti wa Ibaadh ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Amani Mkoa Mwanza, Nuoh Mousa, amesema ni vema kuilinda tunu ya amani iliyopo  izidi kuimalika na kuishi kwa umoja na upendo.
 “Nawaomba wananchi  tuendelee kudumisha amani tuliyonayo ili nchi izidi kumalika kwani kufanya hivyo kutasaidia kumuenzi hayati Magufuli,”alisema Mousa.
Hata hivyo  Mlezi wa Kamati ya Amani Mkoa Altaf Mansoor alisema  alipokea taarifa hizo kwa maskitiko makubwa kwani kiongozi huyo alikuwa shupavu,shujaa na mpenda maendeleo kwa wananchi  lakini ni kazi ya mwenyezi mungu  haina budi kumshukru  na kumuombea dua kwa mema aliyofanya.
“Nimepokea taarifa za msiba huu kwa maskitiko  makubwa kwani tumepoteza Kiongozi shupavu  shujaa lakini  kwa sababu kila mtu aliyezaliwa  lazima atakufa inabidi tumuombee kwa mwenyezi mungu sanjari na  kumpongeza Rais Suluhu Hassan  aliyeshika nafasi hiyo kama katiba inavyosema,” alisema Mansoor.
Mwili wa HHayati Dk. Magufui unatarajiwa kuagwa Jumatano Machi 24, katika Uwanja wa CCM kirumba jijini Mwanza baada ya kuagwa kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar.