26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

MUJATA yaomboleza kifo cha hayati Rais Magufuli


Na Sheila Katikula, Mwanza

Shirika la Mfumo na Muungano  wa Jamii Tanzania (MUJATA) na wadau mbalimbali wameungana na Watanzania wote nchini kuombeleza kifo cha aliyekuwa Rais wa  Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati, Dk John Magufuli, aliyefaliki dunia Machi 7, mwaka huu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanachama hao wamesema watamkumbuka hayati Rais  Magufuli kwa utendaji wake wa kazi na kuwathamini wanyonge.

Naye Mwenyekiti wa  Democrasia Kanda wa Shirika hilo, Clement Pancras, amesema ni vema viongozi waliopo kuendelea kushirikiana na Rais Samia Suluhu Hassan ili kuweza kuendeleza mikakati iliyoachwa na hayati Dk John Magufuli.

Kwa upande wake Katibu wa  MUJATA Mkoa wa Mwanza, Lazaro Simon, akisoma taarifa iliyoandaliwa na shirika hilo amesema hayati Rais Magufuli  ni  miongoni mwa wanamjata kwa sababu   alifanya kazi na jamii ya kulitumikia taifa kwa  uaminifu na upendo.

Aidha, Wakili waTaifa wa Shirika  hilo,Remigius  Mainde amewaomba watanzania   kuwa wavumilivu  katika kipindi cha matatizo ya msiba huo sanjari na kumpongeza Rais aliyeteuliwa kuziba nafasi  hiyo.

Mwenyekiti wa Bajaji Mkoa Mwanza, Valentine Tarimo, amesema alipokea taarifa ya  msiba huo kwa maskitiko makubwa kwani Rais huyo alikuwa  mtetezi wa wanyonge mpenda haki na maendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Nera, Abubakari Seif, amesema kazi ya mwenyezi mungu haina makosa na haisahihishwi  ikifika unashukuru Mungu hivyo ni vema watanzania kukubali tukio hilo na kuwa wamoja na kuvumiliana na kushikamana ili kuwa kitu kimoja

“Nilipokea taarifa ya kifo hiki kwa maskitiko makubwa kwa sababu Magufuli ninamfahamu vizuri kwani tumesoma wote sekondari kwenye shule ya Nyakahoja  alikuwa  ni  jemedari tangu huko nyuma,” amesema Seif.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles