21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Muleba watakiwa kuunga mkono mradi wa bomba la mafuta

Na Renatha Kipaka, Muleba

Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Toba Nguvila amefanya ziara katika maeneo yatakayopitiwa na mradi wa bomba la mafuta na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo ya Kata za Ngenge na Burungura.

Hata hivyo akizungumza na wananchi hao Desemba 13, 2021 kupitia mikutano ya hadhara kwa nyakati tofauti, Nguvila amewataka wananchi wa maeneo hayo kuupokea mradi huo na kutumia fursa mbalimbali kama uuzaji wa mazao, shughuli za mama lishe na ajira.

“Tupo tunapita na kukagua maeneo yatakayopitiwa na mradi wa bomba la mafuta. Nyinyi wananchi ni wanufaika wa mradi huu wa bomba la mafuta, kutakuwa na fursa nyingi kama za mama lishe, vijana mtapata ajira za uchimbaji wa mitaro na vijana mliopita mafunzo ya mgambo mtapata ajira za ulinzi. mradi utakapoanza,” ameeleza Nguvila.

Mkuu wa Wilaya ya Muleba,Toba Nguvila akizungumza na wananchi(hawapo pichani).

Amesema wilaya ya Muleba ndio wilaya pekee Tanzania inayopitiwa kwa urefu mkubwa sana kuliko zingine zinazopitiwa na mradi huo.

Naye Mratibu wa Mahusiano katika mradi wa bomba la mafuta, Charles Shabi, ameeleza kuwa kwa wale ambao mradi utapita kwenye maeneo yao watachagua kujengewa nyumba au kupewa fedha taslim.

Aidha, Kwa sasa wapo katika hatua ya kutembelea kaya zitakazoguswa na mradi na kuzungumza nao ili waamue kama wanataka wafidiwe kwa kupewa fedha au kujengewa nyumba na baada ya hapo uanze mchakato wa taratibu za malipo.

Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ameambatana na wajumbe wa kamati ya Usalama, wataalam kutoka ofisi ya Mkurugenzi na Mratibu wa Mahusiano katika mradi wa bomba la mafuta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles